Mshauri
wa Jukwaa la Matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo (OFAB),
Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akimkabidhi mbegu ya mahindi ya Wema 2109,
Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Bukombe, Joseph Bachibya kwa ajili ya kupanda
katika shamba darasa katika Kijiji cha Msasa kilichopo Kata ya Runzewe
wilayani humo leo. Wengine kutoka kulia ni Mtafiti wa Mazao ya Mizizi
kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas
Kibula na Mtafiti, Dk. Beatrice Lyimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
Maofisa
Ugani wakiandaa shamba darasa la mahindi ya Wema katika Kijiji cha
Kabagole kilichopo Kata ya Busonzo litakalosimamiwa na Kikundi cha Igembensabho.
Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Bukombe, Joseph Bachibya, akizungumza na wakulima wa Kikundi cha Igembensabho.
Wanakikundi cha Igembensabho wakiwa wameshosha mikono ikiwa ni ishara ya mshikamano.
Mshauri
wa Jukwaa la Matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo (OFAB),
Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akimkabidhi mbegu ya mhogo aina ya
Mkombozi, Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Bukombe, Joseph Bachibya kwa ajili
ya kupanda katika shamba darasa katika Kijiji cha Msasa kilichopo Kata
ya Runzewe wilayani humo leo. Wengine kutoka kulia ni Mtafiti wa Mazao
ya Mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera,
Jojianas Kibula na Mtafiti, Dk. Beatrice Lyimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
Ofisa
Kilimo wa Wilaya ya Bukombe, Joseph Bachibya akikmabishi mbegu ya Wema
Ofisa Ugani wa Kijiji cha Kabagole, Ponsian Pancras.
Mtafiti
wa Kilimo kutoka Kituo cha Utafiti wa Ilonga mkoani Morogoro, Ismail
Ngolinda, akiwafundisha wakulima wa Kijiji cha Kabagole namna ya kupanda
mahindi ya Wema. Kulia ni Ofisa Ugani, David Makabila kutoka Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Katibu wa Kikundi cha Igembensabho, Jacob Nsunzu akizungumza na waandishi wa habari.
Ofisa
Kilimo wa Wilaya ya Bukombe, Joseph Bachibya akikmabishi mbegu ya Wema
Ofisa Ugani wa Kijiji cha Msasa, Mohamed Mwangeni. Katikati ni Mshauri wa Jukwaa la Matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange.
Mtafiti
wa Kilimo kutoka Kituo cha Utafiti Ilonga mkoani Morogoro, Ismail
Ngolinda, akiwafundisha wakulima wa Kijiji cha Msasa, namna ya kupanda
mahindi ya Wema.
Na Dotto Mwaibale, Bukombe Geita
WAKULIMA
wilayani Bukombe Mkoani Geita wameiomba Serikali na wasambazaji wa
mbegu bora za mahindi ya WEMA 2109 yanayostahimli ukame kufikisha mbegu
hizo wilayani humo ili kuweza kutatua changamoto ya mavuno kidogo
wanayoyapata kila mwaka kutokana na mabadiriko ya tabia nchi na wadudu.
Ombi
hilo limetolewa na wana Kikundi cha Igembensabho kwenye Kijiji cha
Kabagole Kata ya Busonzo wilayani Bukombe mkoani Geita wakati wakipokea
mbegu bora za mahindi yaliyozalishwa na Mradi wa WEMA kwa ajili ya
kupanda kwenye shamba darasa la kikundi hicho ili waweze kuyalinganisha
na aina za mahindi wanayolima kila mwaka na mahindi hayo yenye sifa ya
kustahimili ukame yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya
Kilimo (OFAB)
Akizungumza
kwa niaba ya wanakikundi hicho, Adam Kasalamsigwa alisema kuwa kutokana
na sifa walizoambiwa na wataalamu kwenye mahindi hayo yatakuwa mkombozi
kwa wakulima wengi kutokana na aina zingine za mahindi waliyozoea
kupanda kushindwa kutoa matokeo waliyokuwa wakiyatarajia baada ya mvua
kukata mapema kabla mahindi hayajazaa.
“Tunashukuru
mmetuletea mbegu hizi ili tufanye majaribio na kuona jinsi mahindi haya
yanavyostahimili ukame lakini mmetuambia tayari mmeshayafanyia
majaribio kwenye maeneo mengine ya Tanzania na kuonyesha mafanikio
makubwa hivyo hatuna sababu ya kusubiri hadi msimu ujao tuleteeni mbegu
hizo tununue na kupanda” alisisitiza Kasalamsigwa.
Aidha
wakulima hao wameiomba Serikali kuona sababu ya kuziingiza mbegu hizo
kwenye ruzuku ya pembejeo ili ziweze kuwafikia hadi vijijini kwa bei
nafuu ili ziweze kukinzana na mabadiliko ya taba nchi ambayo yamekithiri
sana kwenye wilaya hiyo na maeneo mengine.
Akitoa
maelekezo ya namna ya kupanda mahindi hayo Mtafiti kutoka Kituo cha
Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Ismail Ngolinda aliwaambia
mahindi hayo baada ya kufanyiwa utafiti kupitia mradi wa mahindi
yanayotumia maji kwa ufanisi (WEMA) waliyajaribu kwenye maeneo
mbalimbali kwenye mikoa ya Morogoro na Tanga na kuonyesha kufanya vizuri
kuliko aina nyingine za mahindi wanayolima wakulima.
Ngolinda
aliwasisitiza kuwa pamoja na wao kupata mbegu hizo zinazostahimili
ukame lakini ni lazima wazingatie kanuni bora za kilimo cha mahindi
ikiwemo matumizi ya mbolea za kupandia na kukuzia ,kupanda kwa mistari
na nafasi na kufanya Palizi lakini wasipofanya hivyo hawawezi kupata
mavuno yanayostahili badala yake watapata hasara kama mahindi mengine.
Aliwataka
kuzingatia suwala la kupanda kwa mistari na nafasi ili kuweza
kumshakikishia mkulima anatumia shamba lake vizuri badala ya kupanda
holela na kujikuta amepanda miche michache kwenye shamba akidhani ni
ekari moja kumbe ni miche inayoenea kwenye nusu ekari iliyopandwa
vizuri.
Ngolinda
aliwashauri wakulima kulima ekari moja kitaalamu na kwa kuzingatia
kanuni bora za kilimo ili apate mavuno makubwa badala ya kulima ekari
tano ambazo anatumia nguvu nyingi na gharama kubwa lakini mwishoni
anapata mavuno sawa na mtu mwenye ekari moja.
“
Unalima ekari tano bila kufuata kanuni bora za kilimo alafu unapta
magunia 25 ya mahindi wakati mwenzako analima ekari moja tuu kwa kufuata
kanuni bora za kilimo na anapata hadi gunia 30 hii ni tofauti kubwa
sana kwa hiyo wakulima naomba mbadilike” alisistiza Ngolinda.
Aidha
Mtafiti huyo wa zao la mahindi aliwaambia kuwa kufanya majaribio hayo
kupitia mashamba darasa kwenye mkoa mzima wa Geita ni kutaka kuwaonyesha
wakulima hao mbinu za kisasa za kilimo na matumizi ya mbegu bora
yanavyoweza kumsaidia mkulima kuzalisha kwa tija ili aachane na kilimo
cha mazoea ambacho hamkimsaidii mkulima kuondokana na umasikini lakini
kupata chakula cha kutosha.
Awali akizungumza na watafiti hao kutoka COSTECH, Kituo cha Utafiti wa Kilimo Ukiriguru Mwanza na Maruku mkoani Kagera kabla
ya kwenda kutembelea mashamba darasa na kufanya uzinduzi huo kwenye
wilaya hiyo ,Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Dionis Myinga
ameishukuru COSTECH na OFAB kwa kusaidia kutafuta ufumbuzi wa matatizo
ya wakulima kwa kuwapelekea mbegu hizo bora ambazo zinajibu changamoto
mbalimbali sugu za wakulima.
Myinga
alisema sio wataalamu hao wametembea umbali mrefu kutoka Dar es salaamu
hadi Geita ili kufikisha matunda ya utafiti kwa wakulima hivyo wilaya
yake itafanya kazi bega kwa bega katika kuhakikisha malengo ya mpango
huo yanafikiwa ili kuchochea uzalishaji wa mazao hayo kupiti mashamba
darasa hayo.
“Tafiti
zipo nyingi sana kwenye vituo vya utafiti na vyuo vikuu lakini zinabaki
kwenye makabati tuu na hazitumiwi kwenye kutatua tatizo lililokusudiwa
lakini kila utafiti ungefika kwa mlengwa naamini Tanzania tungekuwa
mbali sana kwenye mambo mbalimbali hususani kilimo” alisema Myinga.
Katika
kuonyesha kuridhika kwake na maelezo ya mbegu za mahindi na mihogo
iliyoletwa kwenye wilaya yake akaomba mbegu za kununua za mihogo hiyo
aina ya Mkombozi za kutosha kupanda shamba la ekari kumi ili iwe mfano
kwa wakulima wilayani humo pamoja na kuwa chanzo cha kusambaza mbegu
nyingi kwa wakulima wengi zaidi.
Vijiji
vilivyonufaika na uanzishwaji wa mashamba darasa katika wilaya hiyo ni
Kijiji cha Msasa na Kabagole ambapo mashamba hayo yatasimamiwa na
vikundi.
Watafiti hao kesho siku ya Ijumaa wanatarajia kwenda Halmshauri ya Mji wa Buchosa Sengerema kwa ajili ya kazi ya kuanzisha mashamba darasa na kisha wiki ijayo kwenda kumalizia kazi ya kusambaza mbegu hizo Mkoa wa Tabora.
Watafiti hao kesho siku ya Ijumaa wanatarajia kwenda Halmshauri ya Mji wa Buchosa Sengerema kwa ajili ya kazi ya kuanzisha mashamba darasa na kisha wiki ijayo kwenda kumalizia kazi ya kusambaza mbegu hizo Mkoa wa Tabora.
0 comments:
Post a Comment