METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, November 7, 2017

MAVUNDE AWAPA NEEMA WAJASIRIAMALI DODOMA MJINI

Mbunge wa Dodoma mjini na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde akifungua semina ya wajasiriamali Dodoma

 Washiriki wa semina ya ujasiriamali

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini leo amefungua semina ya wajasiriamali wapatao 2000 wa Jimbo hilo.

Semina hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Cavilam wilayani Dodoma ambapo wajasiriamali hao watapata nafasi ya  kujifunza juu ya elimu ya Ujasiramali na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.

Aidha amesema kupitia semina hiyo watatoa walimu 205 ambao watazunguka katika kata zote 41 za Dodoma Mjini kwenda kufundisha vikundi vya wakinamama,Vijana na Wazee katika masuala ya utengenezaji bidhaa na kuongeza thamani,Ufugaji wa Kuku, Samaki na Mafunzo ya kilimo Bora.

Mavunde amesema baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo litaandaliwa kongamano lingine kubwa litakalohusisha Taasisi za fedha na Mifuko ya Uwezeshwaji ili wajasiriamali wapate fursa ya kufahamu namna ya kuifikia mikopo na ruzuku zitakazosaidia upatikanaji wa mitaji ya kufanyia shughuli za uzalishaji mali.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com