Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa
vyombo vya dola vinatakiwa kupewa muda kwaajili ya kufanya uchunguzi
katika matukio mbalimbali ya mashambulizi dhidi ya wananchi na viongozi.
Ameyasema
hayo hii leo Bungeni Mjini Dodoma, wakati wa maswali na majibu mara
baada ya kuulizwa swali na kiongozi wa kambi rasmi bungeni, Freeman
Mbowe kuhusu kurusu vyombo vya kimataifa kufanya uchunguzi wa tukio la
kushambuliwa kwa mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu
“Suala
hili la kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ni
muendelezo wa matukio ambayo yamekuwa yakitokea sehemu mbalimbali
nchini, ikiwemo mkoa wa Pwani katika Wilaya za Mkuranga, Rufiji na
Kibiti, hivyo, vyombo vya dola vipewe muda wa uchunguzi ili kuwabaini
waharifu,”amesema Majaliwa
Hata
hivyo, ameongeza kuwa Tundu Lissu ni mbunge mwenzao hivyo suala hilo
linamhusu kila mbunge wa kutoka upande wowote, hivyo linashughulikiwa
kama matukio mengine yanavyoshughulikiwa.
0 comments:
Post a Comment