Robo
Fainali ya Kombe la SPANEST Piga Vita Ujangili, Okoa Tembo imeendelea leo kwa
michezo miwili iliyowakutanisha Kinyika FC dhidi ya Ilolompya huku Mboliboli FC
ikicheza na Itunundu FC.
Mchezaji
Hamis Mkosa wa Kinyika FC emeendelea
kutikisa nyavu za wapinzani wake kwa kuipatia timu yake ushindi wa 1-0 dhidi ya
Ilolompya, bao lililofungwa katika Dk 18 katika mchezo uliovunja rekodi ya watazamaji.
Bao
hilo linamfanya Mkosa na Emanuel Sade wa Mapogolo FC kuongoza katika ligi hiyo
kwa kwa kuwa na magoli matano kila mmoja hadi sasa.
Katika
mechi yao ya kwanza Sade aliweka rekodi katika hatua ya robo fainali ya
michuano hiyo kwa kufunga magoli matatu pekee yake katika mechi ambayo timu
yake ilicheza na Mahuninga jana.
Katika
mechi nyingine iliyochezwa leo, Mboliboli na Itunundu wameshindwa kuonesha
ubabe baada ya kulazimishana sare ya bila kufungana katika dakika 90 za mchezo.
Hatua
hiyo ya robo fainali inaendelea kesho kwa mechi za kwanza za marudio zitakazoikutanisha Idodi Vs Malizanga na Mapogolo Vs
Mahuninga.
Mratibu
wa SPANEST, Godwell Ole Meing’ataki amesema mshindi wa kwanza wa kombe hilo
atapata seti moja ya jezi, mipira miwili, cheti, medali ya dhahabu, Sh Milioni
moja taslimu na safari ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Mshindi
wa pili atapata mpira mmoja, cheti, medali ya shaba, na fedha taslimu Sh
700,000 huku mshindi wa tatu akiondoka na mpira mmoja, cheti, medali na fedha
taslimu Sh 500,000.
Amesema
mshindi wa nne wa mashindano hayo atapata mpira mmoja, cheti, na fedha taslimu
Sh 300,000 huku mfungaji bora akiondoka na mpira mmoja na Sh 100,000 na
muazuzi bora akiondoka na jezi na Sh 100,000.
Amesema
ligi hiyo inayofanyika kwa mwaka wa nne sasa ilianzishwa na Spanest ambao ni
Mradi wa Kuboresha Mtandano wa Maeneo Yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania
ikilenga kuwahamasisha wananchi wa vijiji 24 vya tarafa hizo zinazopakana na
hifadhi ya Taifa ya Ruaha kushiriki katika vita dhidi ya ujangili na kuokoa
maisha ya Tembo.
0 comments:
Post a Comment