Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akiongea na wananchi wa Kata ya Kwamgwe wakati akikabidhiwa zahanati iliyojengwa kwa hisani ya shirika la maendeleo la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na nguvu za wananchi, mkuu wa wilaya aliwaomba wananchi waendelee na moyo wa kujitokea katika kuchangia kazi za maendeleo ili kijiji kiweze kujikwamua kimaendeleo. PICHA NA KAJUNASON/MMG – HANDENI, TANGA.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin
Gondwe akimsaidia Diwani wa Kata ya Kwamgwe, Sharifa Abebe alipokuwa
akitoa machozi ya shukrani kwa shirika la maendeleo la World Vision
Tanzania kwa kuweza kushirikiana na wananchi kuwajengea jengo la
zahanati lililoweza kugharimu shilingi milioni 190 ambapo wao World
Vision Tanzania waliweza kutoa Milioni 100 na wao wananchi waliweza
kujitoa kwa nguvu zao kwa thamani ya milioni 90. Hafla hiyo ilifanyika
katika Kata ya Kwamgwe ambapo ndipo jengo hilo lilipojegwa.
Mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP
wa World Vision Tanzania, Humphrey Bernard akisoma risala ya mradi wa
ujenzi wa zahanati iliyojengwa katika Kata ya Kwamgwe ambapo
aliwashukuru wananchi wa kata ya Kwamgwe kwa kuweza kujitoa kufanikisha
ujenzi wa jengo la zahanati.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin
Gondwe akikabidhiwa mikataba wa zahanati na mwezeshaji wa mradi
Mkumburu ADP wa World Vision Tanzania, Humphrey Bernard (kushoto) ambao
ndiyo waliojenga kwa kushirikiana na wananchi waliojitoa kwa hali na
mali.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Handeni, William Makufwe akitoa ufafanuzi jinsi wananchi
walivyoweza kujitoa ujenzi wa zahanati.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya
Wilaya ya Handeni, Dokta Credianus akitoa nasaha zake kwa wananchi wa
Handeni waweze kujua umuhimu wa kuwekeza katika afya.
Jengo la zahanati iliyojengwa katika Kata ya Kwangwe, Wilayani Handeni.
Jengo la zahanati iliyojengwa katika Kata ya Kwangwe, Wilayani Handeni.
Wakati huo huo, mkuu wa wilaya ya
Handeni, Godwin Gondwe akipokea zawadi ya kuku kutoka wa mwenyekiti wa
kitongoji cha Migombani, Michungwani-Segera Bi. Amina Njama ambaye
amekuwa msitari wa mbele katika uhamasishaji wa kukusanya matofali ili
yaweze kusaidia katika ujenzi wa madarasa na zahanati.
Mkuu wa Wilaya akifurahi na viongozi.
Mkuu wilaya akipata maelezo
machache kutoka kwa wananchi waliitikia wito wa kuchangia maendeleo kwa
kuchimba msingi wa zahanati ya Migombani, Michungwani – Segera.
Mkuu wa Wilaya akiwashukuru wananchi kwa moyo wao wa kujitolea katika maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin
Gondwe amewataka wananchi wa Kata ya Kwamgwe kuendelea kujitoa
kikamilifu katika kuchangia shughuli za kijamii ili kuendana na kasi ya
rais Dkt. John Magufuli katika kuleta maendeleo endelevu.
Akizungumza na wakazi wa Kata ya
Kwamgwe wakati akikabidhiwa zahanati iliyojengwa kwa hisani ya shirika
la maendeleo la World Vision Tanzania, mkuu wa wilaya aliwaomba wananchi
waendelee na moyo wa kujitolea katika kuchangia kazi za maendeleo ili
kijiji kiweze kujikwamua.
“Nawaomba ndugu zangu, sisi wote
ni wanaKwamngwe, lazima tuamue kuchangua mambo muhimu matatu, kutambaa,
kutembea au kukimbia. Jambo la msingi ni lazima tuwe katika mwendo,
tuendelee kujitoa tuzidi kuleta maendeleo kijijini kwetu,” alisema
Gondwe.
Awali akikabidhi mradi huo wa
zahanati hiyo, Mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP, Humphrey Bernard
aliwashukuru wananchi wa kata ya Kwamgwe kwa kuweza kujitoa kufanikisha
ujenzi wa jengo la zahanati.
Wakati huo huo, Mkuu wa wilaya
Handeni aliweza kutembelea ujenzi wa kituo cha afya cha Michungwani,
Segera ambapo ujenzi wake unaanza hivi karibuni kwa nguvu za wananchi
kupitia kampeni ya mkuu huyo ya kuongeza zahanati na madarasa.
0 comments:
Post a Comment