KAMPUNI
ya bia nchini ya TBL imepewa tuzo ya kwanza ya matumizi bora ya magari
makubwa ya mizigo ya Mercedes Benz Actros ambayo yametimiza zaidi ya
kilomita milioni moja huku yakiwa bado katika hali bora.
TBL ina magari kumi ya aina hiyo ambayo yamefanya kazi kwa miaka 17.
Tuzo
hiyo imetolewa na DAIMLER kwa kushirikiana na kampuni tanzu ya CFAO
nchini Tanzania ambayo ndiyo mawakala pekee wa magari ya Mercedes Benz
nchini Tanzania.
Tuzo
hiyo Mercedes-Benz Actros yenye kubeba jina la ‘Mileage Millionaire’
kutokana na kupita kilomita milioni moja, imetolewa kuonesha kuridhishwa
kwa watengenezaji wa magari hayo juu ya uimara wake. TBL ina magari
zaidi ya 80 ya Mercedes Benz.
Magari
yote hayo yamefikisha kilomita milioni 11 katika miaka 17 ya kuwa
barabarani. Kilomita hizo ni sawa na kuzunguka dunia mara 275.
Gari
linaloongoza katika ‘Mileage Millionaire’ ni Actros modeli ya 3340,
ambalo limefikisha kilomita 1,519,459 tangu lilipoingizwa TBL mwaka
2000. Magari mengine ni Actros za mwaka 2002,2003 na 2004 zikiwa na
wastani wa kilomita kati ya kilomita milioni 1.02 na 1.5.
Magari
hayo yamekuwa yakitumika katika njia zote za Tanzania kupeleka vinywaji
kutoka Dar es salaam, Arusha na Mwanza kwenda maeneo mbalimbali ya
Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa magari yote hayo yalinunuliwa moja kwa moja kutoka CFAO Motors Tanzania.
Bosi
wa magari ya kibiashara ya Daimler upande wa Afrika, Naeem Hassim
alisema katika kukabidhi tuzo hizo kwa TBL kwamba kuwa na magari ya aina
hiyo katika kampuni yake kufikisha zaidi ya kilomita milioni 1 na bado
yakiwa ‘vijana’ si jambo la kushtusha kwa Mercedes-Benz Actros.
Alisema
Actros yamejitanabaisha kwa ubora wake na kuaminika kwake:” ni dhahiri
kuwa na magari kama haya ni uwekezaji wenye maana kubwa, ni vyema wateja
wakayambua kwamba Actros ni gari la kuaminika.”
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo alisema
katika utoaji tuzo huo kwamba wanafurahi sana kusherehekea kilomita
zaidi ya milioni moja ya magari ya ACTROS.
Alisema
ni mafanikio makubwa kuwa na magari hayo na hiyo inamaananisha kwamba
ni imara na yanayoaminika yakiwa yametengenezwa kuhimili hali mbaya
zaidi na kwamba wateja wanaweza wakawategemea kwa huduma bora za mauzo
na pia uhudumiaji wa gari lenyewe ili liweze kudumu zaidi.
Akipokea
tuzo hiyo mwakilishi wa Tanzania Breweries Limited, ambaye ni meneja wa
lojistiki wa Afrika Mashariki James Nyoike alisema kwamba amefurahi
sana kuwa sehemu ya simulizi lenye mafanikio katika uendeshaji wa
kampuni kwa kuwa na magari yenye sifa kubwa wa uimara.
Alisema
anafurahia huduma ya matengenezo inayopata magari yake kila
yanapotakiwa kutengenezwa, pamoja na mafunzo kwa madereva hali
iliyowezesha kuwapo kwa udumu zaidi kwa magari.
“Tuna zaidi ya magari 80 ya Mercedes Benz kuanzia modeli za 2000 hadi
2016. Magari haya yamethibitisha ubora wake kazini na kuwa sehemu muhimu
sana ya kazi zetu hasa za usambazaji wa bidhaa” alisema Nyoike.
Katika
mahojiano alisema kwamba gari lililopitisha kilomita milioni 1.5 T 418
AAT limeendeshwa na dereva mmoja Moses Ulenga kwa miaka 10.
“Nasikitika kwamba hakuhudhuria sherehe hizi, yuko safari”
alisema Nyoike ambaye alisema pamoja na kufuata utaratibu wa service wa
gari pia wamekuwa wakifanyia matengenezo ya kuzuia uharibifu na kwamba
madereva wake wamefunzwa na zipo taratibu za kufuata zenye kuonesha
nidhamu ya barabara.
Naye
Tharaia Ahmed Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko amesema kwamba wamemua
kutoa tuzo hiyo kwa TBL kama sehemu ya kuonesha namna gani ushirikiano
kuanzia mauzo hadi matunzo unavyoweza kumnufaisha mtu ambaye ananunua
magari hayo kutoka CFAO.
Alisema
TBL imeonesha ubora wa magari hayo na kuaminika kwake katika safari
ambazo wakati mwingine ni ngumu sana kwa kuzingatia mazingira vyetu.
CFAO
Motors Tanzania ambayo zamani ilijulikana kama DT Dobie ni kampuni
tanzu ya kundi la makampuni ya CFAO ya Ufaransa. CFAO Motors iliundwa
1952na ni wakala wa magari mbalimbali Mercedes-Benz ya kibiashara, ya
abiria na ya binafsi.
0 comments:
Post a Comment