Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla amesema Tanzania na
Nchi ya Oman wamefanya mazungumzo ya pamoja ya namna ya kukuza sekta ya
Utalii baina ya nchi hizo mbili ambapo watashirikiana katika
muingiliano wa Watalii watakaokuwa wakitokea moja kwa moja Oman na kuja
Tanzania.
“Tumeweza
kuzungumzia ushirikiano wa sekta ya Utalii. Hii ni pamoja na kuanzisha
soko la pamoja kati ya Oman na Tanzania. Watalii wanaokwenda Oman
wanaotaka kuja nchi za Afrika basi waunganishwe moja kwa moja kutoka
Oman na kuja Tanzania kwani wenzetu wana watalii wengi kuliko sisi.
Hivyo ujio wao hapa nchini ni faida kubwa kabisa na tumejifunza mengi
katika sekta hii.
"Pia
tumeweza kujifunza namna wenzetu wanavyoitangaza nchi yao na sisi
tutatumia uzoefu huo kuboresha sekta hii ya Utalii kama dhamana
tuliyopewa” alieleza Dk. Kigwangalla.
Awali
Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa
Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’ iliyofika mapema jana Jijini
Dar e Salaam ikiwa katika msafara wa kitaifa kati ya Serikali ya Oman
na Tanzania.
Aidha,
katika tukio hilo Mh. Waziri DK. Kigwangalla aliweza kuungana na Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mama Samia Suluhu
Hassan katika chakula cha mchana ndani ya Meli hiyo ya Mfalme wa Oman
Mhe. Qaboos bin Said ijulinakanyo kama ‘Fulk Al Salamah’.
Meli
hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al
Salamah’ ipo nchini hadi Oktoba 21.2017. ambapo ipo nchini kusambaza
ujumbe wa ‘Amani na upendo’ duniani ambapo ikitoka Tanzania inatarajia
kuelekea Mombasa Kenya kwa madhumuni hayo hayo.
Moja ya alama za kuvutia za Taifa la Oman
Moja ya usafiri unatumika katika nyanja za Utalii nchini Oman
0 comments:
Post a Comment