Waziri mkuu wa Uhispania Mariano
Rajoy, anasema analivunja bunge la Catalonia na kuitisha uchaguzi wa
mapema baada ya eneo hilo kujitangazia uhuru.
Waziri mkuu alisema kuwa udhibiti kamili kwa eneo hilo ni muhimu katika kurejesha hali ya kawaida. Anamfuta kazi kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont na baraza lake la mawaziri
Mapema bunge la Catalonia lilipiga kura kwa wingi kujitangazia uhuru.
Mzozo huu ulianza wakati watu wa Catalonia waliunga mkono uhuru kwenye kura iliyokumbwa na utata mapema mwezi huu.
- Uhispania yatoa vitisho kwa Catalonia
- Viongozi wa Catalonia wazuiwa rumande Uhispania
- Catalonia kujitangazia uhuru karibuni
Bunge la Senate la Uhispania liliipa serikali ya Bw. Rajoy mamlaka ya kikatiba kufuta uhuru wa Catalonia na baada ya mkutano wa baraza la mawaziri Bw. Rajoy alisema kuwa hilo litafanyika
Catalonia ilisema kuwa asilimia 43 ya watu walioshiriki katika kura hiyo asilimia 90 waliunga mkono uhuru.
Lakini mahakama ya katiba nchini Uhispnaia imeitaja kura hiyo iliyo kinyume na sheria.
0 comments:
Post a Comment