Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Morogoro mjini Abdulaziz Abood
pamoja na Mkuu wa wilaya ya Morogoro wakifanya ukaguzi wa barabara
zinazojengwa kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa barabara za lami Manispaa ya Morogoro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya
Morogoro wakikagua maandalizi ya ujenzi wa barabara za lami
zinazoendelea kujengwa.
Meneja wa Tarura Manispaa ya
Morogoro akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi
Selemani Jafo alipotembelea kukagua maandalizi ya ujenzi wa barabara za
lami.
…………….
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amemtaka meneja wa Wakala wa Barabara
Vijijini(TARURA) Manispaa ya Morogoro kuhakikisha barabara za lami
zinazojengwa ndani ya manispaa hiyo zinakuwa katika ubora unaotakiwa ili
ziweze kudumu kwa muda mrefu.
Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa
akikagua miradi ya ujenzi wa barabara hizo huku akibaini kuharibika kwa
baadhi ya barabara za lami zilizojengwa miaka michache iliyopita.
Amesema kuwa ujenzi wa barabara za
lami umekuwa ukitumia gharama kubwa hivyo ni vyema Meneja huyo
akahakikisha anasimamia ili ujenzi wake uwe kwenye viwango
vinavyotakiwa.
“Haiwezekani tunatumia fedha
nyingi lakini barabara zinaharibika ndani ya muda mfupi wakati wahandisi
mnaosimamia mpo.Sitamvumilia mhandisi yeyote kwa miradi inayojengwa
endapo haitakidhi viwango,”amesema Jafo.
Jafo amewaonya mameneja ya TARURA
wa wilaya ambao watashindwa kusimamia kazi zao ipasavyo katika
halmashauri zao wanazozisimamia kuwa serikali haitasita kuwachukulia
hatua.
0 comments:
Post a Comment