Wafanyakazi
wa Benki ya NMB ,Matawi ya Mawenzi na Mbuyuni wakiwa katika Hospitali
ya St,Joseph mjini Moshi kwa ajili ya zoezi la usafi pamoja na kutoa
zawadi kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo ikiwa ni muendelezo
a wiki ya huduma kwa wateja.
Mmoja
wa watumishi wa Hosptali ya St Joseph akimvisha kizuia vumbi
,mfanyakazi wa Benki ya NMB walipofika hospitalini hapo kwa ajili ya
kufanya usafi.
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya St Joseph Sista,Ubanus Lyimo akimvisha kofia
maalumu Menenja wa Benki ya NMB,tawi la Mawenzi kabla ya kuanza zoezi la
Usafi katika Hospitali hiyo.
Wafanyakazi
wa Benki ya NMB,matawi ya Maeenzi na Mbuyuni mjini Moshi wakishiriki
zoezi la usafi eneo la nje ya Hospitali ya St Joseph ikiwa ni sehemu ya
kuendelea na maadhimisho ya wiki ya huduma kwa watena.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakichoma moto taka mara baada ya kuhitimisha zoezi la usafi katika Hospitali hiyo
Wafanyakazi
wa NMB,matawi ya Mawenzi na Mbuyuni mjini Moshi ,wakiwa wameshikilia
Fagio mara baada ya kuhitimisha zoezi la usafi katika Hospitali ya St
Joseph.
Afisa
Mikopo katika Benki ya NMB,tawi la Mawenzi mjini Moshi,Elikana Boyi
akikabidhi mche wa sabani kwa mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika
hospitali ya St Joseph Mjini Moshi.
Meneja
wa NMB,tawi la Mawenzi ,Johnson Urasa akiweka mche wa sababuni mbele ya
mtoto aliyelazwa katika hospitali ya St Joseph ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya huduma kwa wateja.
Meneja
wa Benki ya NMB,tawi la Mbuyuni ,Rose Manyoni (katikati) akisaidiana na
mwenzake kumuinua mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya St
Joseph walipofika kuwajulia hali pamoja na kutoa zawadi.
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya St Joseph ya mjini Moshi,Sista Ubanus Lyimo
akizungumza mara baada ya Wafanyakazi wa Benki ya NMB,matawi ya Mawenzi
na Mbuyuni kuhitimisha zoezi la kutoa zawadi kwa wagonjwa
waliolazwakatika hospitali hiyo.
Meneja
wa Benki ya NMB,tawi la Mawenzi ,Johnson Urasa akizungumza mara baada
ya kuhitimisha zoezi la kufanya usafi pamoja na utoaji wa zawadi kwa
wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo.
Wafanyakazi
wa Benki ya NMB,matawi ya Mawenzi na Mbuyuni wakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya kuhitimisha zoezi la kufanya usafi na utoaji wa
zawadi kwa wagonjwa waliolazwakatika Hospitali ya St Joseph ya mjini
Moshi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
0 comments:
Post a Comment