METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, October 20, 2017

Wafanyakazi Wa TDL Wapatiwa Mafunzo Ya Ujasirimali Na Nidhamu Ya Fedha

KONYAGI FINANCIAL TRAINING 1
Mkufunzi kutoka  kampuni ya Cornerstone,David Christian, akibadilishana mawazo na baadhi ya  wafanyakazi wa TDL
KONYAGI FINANCIAL TRAINING 8
Baadhi ya wafanyakazi wa TDL wakimsikiliza kwa makini mtaalamu wa masuala ya fedha kutoka kampuni ya Cornerstone.Elvis Kato,wakati wa mafunzo hayo
KONYAGI FINANCIAL TRAINING 11
Baadhi ya wafanyakazi  wa TDL wakifuatilia mafunzo kutoka kwa wakufunzi
……………..
Kampuni ya Tanzania Distillers Limited (TDL)  iliyopo chini ya kampuni mama ya TBL Group imewezesha wafanyakazi wake kupata mafunzo ya mbinu za biashara na matumizi mazuri  ya fedha ambayo yametolewa na wataalamu kutoka kampuni ya masuala la ushauri na mafunzo ya biashara ya Cornerstone Partners ya jijini Dar es Salaam.
 
Mafunzo hayo ya wafanyakazi ni mwendelezo wa  mkakati wa kampuni ya TBL Group wa kuwapatia wafanyakazi wake mafunzo mbalimbali  ya nje na ndani ya kampuni lengo kubwa likiwa ni kuwawezeha kupata ujuzi wa kufanya kazi zao kwa ufanisi sambamba na maarifa ya kukabiliana na changamoto mbalimbali  katika maisha yao ya kila siku.
 
Masuala ambayo walifundishwa ni kuhusiana na mipango ya matumizi ya fedha,jinsi ya kujiwekea akiba na kufanya uwekezaji wenye tija,kupanga kuendeleza taaluma zao,ujasiriamali  na jinsi ya kulinda mali walizonazo zisipotee bila mpangilio.
 
Wakiongea baada ya kumalizika mafunzo,baadhi ya wafanyakazi walishukuru mwajiri wao kwa kuwaandalia mafunzo ya mara kwa mara ya kuwajenga na kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku kama ambavyo wamepata mbinu mbalimbali kuhusiana na matumzi mazuri ya fedha ,uwekezaji na ujasiriamali.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com