Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini
Anthony Mavunde akishiriki Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya
Darul Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya Dodoma.
Washiriki wa Dua maalum katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya Dodoma
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini
Anthony Mavunde akizungumza katika Dua maalum iliyofanyika katika
Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akiwa kwenye picha na viongozi wa dini
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini
Anthony Mavunde akisikiliza mawaidha katika Dua maalum iliyofanyika
katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe Manispaa ya Dodoma
……………….
Viongozi mbalimbali na waamini wa
dini ya Kiislamu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,wamempongeza Mbunge wa Jimbo
la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde kwa utendaji kazi na kuleta
maendeleo katika Jimbo hilo.
Pongezi hizo zimetolewa leo wakati wa Dua maalum iliyofanyika katika Madrasa ya Darul Mustafa-Chang’ombe.
Viongozi hao wamempongeza Mbunge
Mavunde kwa kugawa vitabu vya Misahafu 50,Juzuu 400 na Kanzu 300 katika
misikiti mbalimbali hapa Dodoma Mjini na kwa kusimamia mabadiliko
makubwa katika sekta za Afya, Elimu, Miundombinu,Michezo na Uwezeshaji
wananchi.
Akitoa maelezo ya awali,Mwalimu wa
Madrasa Ustadhi Omar Salum Itara amemshukuru Mavunde kwa msaada mkubwa
alioutoa katika Madrasa hiyo ikiwa pamoja na kuwawekea umeme ili
kuwawezesha wanafunzi kuendelea kujifunza mpaka usiku.
Kwa upande wake, Mavunde
akizungumza katika Dua hiyo, amewashukuru Viongozi na waamini wa dini ya
kiislamu kwa namna wanavyomuunga mkono katika shughuli mbalimbali za
kuwaletea maendeleo na kuwaomba waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu
atimize majukumu yake vyema.
Mavunde ameipa Misikiti 16 Spika
moja kila mmoja zenye thamani ya Tsh 4,000,000 na pia ameahidi kukabidhi
Laptop 2 zenye thamani ya Tsh 1,000,000 na milango miwili yenye thamani
ya Tsh 500,000 kwa ajili ya madrasa ya Darul Mustafa.
0 comments:
Post a Comment