Ofisa Masoko Mwandamizi wa DSE, Mary Kinabo
Dar es Salaam. Kampuni tatu za nje zimechangia kushuka kwa mauzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa Sh50 bilioni.
Taarifa
ya DSE inazitaja kampuni ambazo hisa zake zimeongoza kushuka kuwa ni
Uchumi Supermarket (USL) kwa asilimia 22, Shirika la Ndege la Kenya (KA)
asilimia 16 na Acacia kwa asilimia tisa.
Mauzo ya soko
hilo kwa kipindi cha wiki moja yameshuka kutoka Sh53 bilioni mpaka Sh3
bilioni baada ya hisa 800,000 za kampuni za ndani kuuzwa kati ya
Septemba 25 hadi Septemba 29.
Wiki iliyoishia Septemba 22, jumla ya mauzo ilikuwa Sh53 bilioni, lakini wiki iliyoishia Septemba 29 yalikuwa Sh3 bilioni.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, USL ilianza wiki ikiuza hisa kwa Sh90 lakini
ikamaliza kwa Sh70 wakati KA ilianza na Sh120 na ikahitimisha kwa Sh100.
Hisa za Acacia ambayo inaendelea na mazungumzo na Serikali baada ya
kuzuiwa kusafirisha mchanga wa madini zilikuwa zinauzwa Sh5,480 mwanzo
mwa wiki hiyo lakini zilishuka mpaka Sh4,980.
Bei ya
hisa za Acacia zimepungua kutoka Sh12,500 kabla ya zuio hilo, Machi
mwaka huu. Wakati suala la mchanga likiitesa Acacia, maduka ya Uchumi
yanakabiliwa na madeni ya bidhaa inazoletewa kiasi cha Serikali ya Kenya
inakotoka kuahidi kuisaidia kuyalipa.
Ofisa Masoko
Mwandamizi wa DSE, Mary Kinabo alisema kupungua kwa hisa zilizouzwa
kutoka milioni nne hadi 800,000 kumechangia kuporomoka kwa mapato hayo.
Hata
ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa sokoni hapo umepungua kwa
Sh115 bilioni. “Wiki iliyoishia Septemba 23 ulikuwa Sh20.5 trilioni
lakini Septemba 29 ulikuwa Sh20.3 trilioni,” alisema Kinabo.
Hata
hivyo, ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umeongezeka kwa Sh71 milioni
kutoka Sh9.6 trilioni hadi Sh9.7 trilioni kutokana na kupanda kwa bei
ya hisa za Kampuni ya Sigara (TCC) iliongoza kwa kwa asilimia 66
ikifuatiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa asilimia 27 na Benki ya
CRDB asilimia mbili.
0 comments:
Post a Comment