Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeadhimisha siku ya
Viwango Dunia kwa kutoa zawadi na vyeti kwa wanafunzi walioshinda
shindano la uandishi wa Insha kama sehemu sehemu ya maadhimisho hayo na
pia kuwajengea uwezo na uelewa wanafunzi juu ya umuhimu wa viwango.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Prof.Egid Mubofu alisema shirika lake linaipa
siku ya viwango duniani kwa kuwajengea uwezo vijana kwa kuwashindanisha
kwenye uandishi wa insha. “Lengo kubwa la maadhimisho haya ni kutoa
elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa viwango katika kuboresha maisha ya
wananchi katika ubora wa vitu vyao, afya , usalama na biashara,” alisema
Prof.Mubofu
Prof. Mubofu alisema kila mwaka Shirika la Viwango Duniani
huwa na Kauli mbinu yake ambayo kwa mwaka huu ni “Viwango huifanya Miji
kuwa ya Kisasa zaidi” ambapo kauli mbiu hii inaweka msisitizo kupitia
viwango uboreshaji wa maisha ya wakazi wa mijini kuwa ya kisasa
zaidi.
“Shirika huandaa mashindano ya Insha katika shule za sekondari
kupitia kauli mbinu ya mwaka ya viwango lengo ikiwa kupima uwezo wa
wananfunzi katika ufahamu wao kuhusu viwango,” alisema Prof.Mubofu
Alisema hii inatoa nafasi ya kupima kwa namna gani wananchi wanaelewa
juu ya umuhimu wa viwango na kipi kifanyike katika kuwajengea uwezo hasa
wanafunzi katika kuelewa juu ya majukumu na umuhimu wa viwango katika
maisha yao.
Prof.Mubofu alisema TBS imetoa zawadi pamoja na vyeti kwa
washindi wa insha ikiwa ni motisha ilikuchochea ushiriki wa wanafunzi
wengine katika mashindano mbalimbali yanayotolewa na shirika kuhusu
umuhimu wa viwanda. Aliongeza kuwa kutoka na ushiriki wa wanafunzi
katika shindano hilo kuwa mkjubwa, TBS imejipanga kuboresha vigezo vya
ushiriki ili kutoa nafasi kwa wanafunzi wa ngazi zote kushiriki
kikamilifu.
“ TBS imejipanga kuboresha maisha ya watanzania kwa
kusimamia viwango vya ubora katika maeneo yote hasa uzalishaji na ujenzi
na afya,” alisema Prof.Mubofu na kuongeza kuwa azma ya serikali ya
awamu ya tano ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda itatekelezeka
kwa kuwa na usimamizi madhubuti wa viwango.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa uandaaji viwango TBS, Bi. Edna Ndumbaro alisema matumaini ya TBS
kupitia mashindano ya insha katika maadhimisho ya siku ya viwango
duniani ni kuwapatia uelewa na elimu kuhusu maswala ya viwango kwa
manufaa ya sasa na jamii ijayo.
“Wanafunzi 10 kutoka Shule za sekondari
za Kibaha,Feza, Elboru na Loyola walipatiwa zawadi ikiwa ni ishara ya
kuifanya elimu ya viwango kuwa endelevu,” alisema Bi.Ndumbaro Mshindi wa
kwanza wa shindano la Insha alikuwa mwanafunzi kutoka shule ya
Sekondari Kibaha,Bw. Barnabas Michael ambaye alisema kushiriki kwenye
mashindano kunamfanya mwanafunzi kujijengea uwezo wa kujieleza na pia
kuwa na ufahamu wa mambo kwa mapana yake.
“Wito wangu kwa wanafunzi
wenzangu ni kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mashindano mbalimbali
kwani yanasaidia kuongeza maarifa na uwezo wa kupambanua mambo
mbalimbali,” alisema Bwana Michael Siku ya Viwango Duniani uazimishwa
kwa lengo la kuelimisha juu ya uelewa miongoni mwa mamlaka za udhibiti,
viwanda na walaji kuhusiana na umuhimu wa viwango kwa uchumi wa dunia
ikiwepo Tanzania.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS) Prof.Egid Mubofu akitoa mada
kwenye hafla ya maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani yaliyofanyika
katika ofisi za shirika hilo Ubungo jijini Dar salaam. Katika
maadhimisho hayo yaliambatana na utoa wa vyeti na zawadi kwa
wanafunzi walioshinda katika shindano la uandishi wa insha uliendana na
kauli mbiu ya maadhimisho ambayo ni “VIWANGO HUIFANYA MIJI KUWA YA
KISASA ZAIDI”
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS) Prof.Egid Mubofu akikabidhi
zawadi ya Laptop, cheti na Kiasi cha shilingi laki tatu na nusu kwa
mshindi wa Kwanza wa uandishi wa Insha mwanafunzi Shule ya
Sekondari Kibaha Bw. Barnabas Michael katika shindano maalum la
kuadhimisha siku ya viwango Duniani ikiwa na kauli mbiu “VIWANGO
HUIFANYA MIJI KUWA YA KISASA ZAIDI” . shindano hilo limelenga wanafunzi
kwa lengo la kuandaa kizazi chenye uwelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa
viwango katika ubora, Afya, Usalama na Biashara.
0 comments:
Post a Comment