Na; Ramadhani Shabani
Ndugu Mtanzania Ni Tumaini Langu Wewe Ni Bukheri Wa Afya Na Unaendelea Vyema Na Utekelezaji Wa Ilani Ya Uchaguzi Ya CCM Haswa Ktk Kusimamia Kauli Mbiu Ya Hapa Kazi.
Ndugu Mtanzania Baada Ya Salama,Leo Nimekuletea Habari Inayohusu Shughuli Za Utekelezaji Wa Majukumu Ya kikazi Ya Mhe Naibu Waziri Wa Maji Na Umwagiliaji Ndugu Jumaa Hamidu Aweso.
Mhe Naibu Waziri Wa Maji Na Umwagiliaji *Ndugu Jumaa Hamidu Aweso* Mapema Leo Tarehe 15/10/2017 Amefanya Ziara Ktk Wilaya Ya Maswa Ambapo Ziara Hiyo Wilayani Maswa Ilimfikisha Moja Kwa Moja Ktk Ukaguzi Wa Ujenzi Wa Mradi Mkubwa Wa Uchimbaji Wa Visima Vya Maji Unaoendelea Ktk Wilaya Hiyo Ya Maswa Mradi Huo Wa Uchimbaji Wa Visima Unakuja Kutokana Na Kukauka Kwa Bwawa Ambalo Lilikuwa Ndio Chanzo Kikubwa Cha Maji Kwa Wananchi Wa Wilaya Hiyo Ya Maswa Mkoani Simiyu.
Mradi Huo Wa Uchimbaji Wa Visima Kwaajili Ya Kuwapatia Maji Safi Wananchi Wa Wilaya Ya Maswa Unatajia Kugharimu Shillingi Milioni Mia Mbili Na Arobaini Na Nane (248 Milioni) Kwa Kila Kisima.
Hata Hivyo Mradi Huo Wa Uchimbaji Wa Visima Vya Maji Safi Kwa Ajili Ya Wananchi Wa Maswa, Unatarajia Kukamilika Mapema Na Kuwa Mwarobaini Mkubwa Kwa Kero Kubwa Ya Maji Ambayo Imekuwa Ikiwakabiri Wananchi Wa Wilaya Hiyo Ya Maswa Na Haswa Kutokana Na Kukauka Kwa Bwawa Kubwa Ambalo Lilikuwa Likitegemewa Kama Chanzo Kikubwa Cha Maji Safi Na Salama Kwa Ajiri Ya Matumizi Ya Wananchi Wa Wilaya Hiyo Ya Maswa.
Uchapakazi,Usikivu Na Uzalendo Ni Nguzo Bora Ktk Ujenzi Wa Tanzania Mpya.Vijana Tukiaminiwa Basi Tusiangushe Matumaini Ya Watanzania Zidi Yetu. Nina Imani Na Vijana Na Sasa Ni Wakati Wa Vijana Mhe Rais Haukukosea Kumuamini Kijana Mwenzetu Mzalendo Ndugu Jumaa Hamidu Aweso.
0 comments:
Post a Comment