Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula Leo ameshuhudia na kuhudhuria kama mgeni rasmi makabidhiano ya gari kwa Timu ya mpira wa miguu kutoka wilaya ya Ilemela mkoa wa Mwanza Mbao Fc inayoshiriki ligi kuu kutoka GF Truck and Equipment kama ishara ya kuunga mkono jitihada za mbunge huyo katika kuinua michezo ndani ya Jimbo lake
Akizungumza katika makabidhiano hayo Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kuahidi kuendelea kuunga mkono Timu hiyo ya Mbao Fc kuhakikisha inafika mbali ikiwa ni sambamba na ukuzaji wa michezo unaoenda sambamba na ukuaji wa uchumi wa wanamichezo hao
'... Niwahakikishie kuwa tutaendelea kuwa pamoja ili kuhakikisha Timu yetu inazidi kufanya vizuri na lengo letu ni kuona ukuaji wa michezo unaoenda sambamba na ukuaji wa uchumi wa wachezaji wetu ...' Alisema
Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula amewataka wadau wengine wa michezo nchini kuiga mfano wa GF Truck and Equipment katika kuunga mkono shughuli mbalimbali za kijamii ili kuiletea maendeleo
Kwa upande wao Uongozi wa Timu ya Mbao Fc umeendelea kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula kwa jitihada zake za tangu awali mpaka ilipofikia sambamba na ukuzaji wa vipaji mbalimbali vya michezo unaoenda sambamba na ukuaji wa uchumi wa wanamichezo wenyewe
' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
18.10.2017
0 comments:
Post a Comment