METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, June 26, 2015

Muhariri wa gazeti la Mawio afariki Dunia

Edson Kamukara enzi za uhai wake

Anaandika Mathias Canal, Iringa

"Mwandishi wa habari, Edson Kamukara
amefariki dunia jana jioni.Taarifa zilizonifikia kutoka kwa Mwanahabari maarufu wa TBC1, Angela Msangi, zinaarifu kuwa Mwandishi huyo aliyepata kuandikia gazeti la Tanzania Daima na baadae kuhamia Mwanahalisi, amefikwa na umauti leo jioni baada ya kulipukiwa na jiko la gesi nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam.

Aidha habari kutoka kwa majirani zinaarifu kuwa Kamukara amerejea kutoka Bukoba, na alijisikia vibaya wakati anaenda dukani kununua dawa akaanguka na majirani kusaidia kumpepea na baade kupelekwa kwake ambako alipumzika hadi alipopata nguvu na kuamua kujiandalia chakula na ndipo ajali hiyo kumfika na kugharimu maisha yake.

Pumzika kwa amani Ndugu yetu Kamukara!" Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii
Neno Langu La Wakati Mwema lajikita sasa kusema nimeguswa na msiba wa mwanahabari huyu ama hakika si muda mrefu sana nikiwa Dodoma, kwenye Redio Mwangaza Fm nikifanya mjadala yeye ni miongoni mwa watu waliokuwa wananipa hamasa ya kujadili na kusema bila kuhisi pengine kutokana na makala ama chambuzi zake.

Kila la kheri katika ukamilisho wa safari yako ama hakika hapa duniani tu wapitaji.
Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu Kamukara. AMEN




Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com