METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, October 20, 2017

Matokeo Darasa la 7 Yatangazwa

Baraza la Mitihani Taifa NECTA limetangaza matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2017, na kusema kuwa ufaulu umeongezeka kwa 2.4% ukilinganisha na ule wa mwaka jana 2016.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa wa NECTA Dkt. Charles Msonde, na kusema kuwa watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 na zaidi, kati ya alama 250 ambazo walitakiwa kupata.

Dkt. Msonde ameendelea kusema kwamba kati ya waliofaulu wasichana ni 341 020 ambayo ni sawa na 70.93% na wavulana ni 321, 015, ambao ni sawa na 74.80%, na idadi ya watahiniwa wote waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76%.

Katibu Mkuu huyo aliendelea kwa kusema kwamba ufaulu  katika masomo ya Kiswahili, Kingereza na Hisabati umepanda kati ya 4.25% na 10.05% ukilinganisha na mwaka jana, huku masomo ya Sayansi na Maarifa ya Jamii ukishuka kati ya 3.56% na 13.97%.

Sambamba na matokeo hayo pia Dkt. Msonde amezitaja shule bora zilizofanya vizuri kitaifa ambazo ni kama zifuatazo

St. Peters - Kagera,

St, Severine - Kagera,

Alliance – Mwanza

Sir. John – Tanga

Palikas – Shinyanga

Mwanga – Kagera

Hazina - Dar es salaam

St. Anne Marie - Dar es salaam

Rweikiza – Kagera

Martin Luther - Dodoma.

Pia Dkt. Msonde amezitaja shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa ambazo ni

Nyahaa – Singida

Bosha - Tanga

Ntalasha – Tabora

Kishangazi – Tanga

Mntamba – Singida

Ikolo – Singida

Kamwala – Songwe

Kibutuka - Lindi

Mkulumanzi – Tanga

Kitwai A – Manyara

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com