Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche
Mwanjelwa (Mb) akizungumza wakati wa kikao cha kazi na Wakuu wa Idara na
Vitengo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa wizara ya Kilimo (Kilimo IV)
Kikao kikiendelea
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utafiti Dkt
Mansoor Hussein
Picha ya pamoja Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe
Dkt Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) (Katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe na wakuu wa Idara na Vitengo mara baada ya
kumalizika kwa kikao cha kazi.
Mkurugenzi wa Utawala na rasilimali watu wa Wizara
ya Kilimo Ndg Seushi Mburi akisoma taarifa fupi ya Wizara ya kilimo
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche
Mwanjelwa (Mb) akitafakari jambo wakati kikao kikiendelea
Na Mathias Canal, Dodoma
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche
Mwanjelwa leo Octoba 26, 2017 amewaagiza watumishi kutofanya kazi kwa mazoea
badala yake kuongeza ufanisi katika kazi kwa kuwa wabunifu, na waadilifu.
Mhe Naibu Waziri ametoa agizo hilo wakati wa kikao
cha kazi alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa wizara hiyo
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa wizara ya Kilimo (Kilimo IV), kwa lengo la
kufahamiana na kujua majukumu ya kila idara na vitengo.
Alisema kuwa ili kutimiza adhma ya serikali ya awamu
ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dokta John
Pombe Magufuli katika kuboresha huduma za wananchi ni lazima watumishi kubadili
taswira ya kufanya kazi kwa mazoea na kuhamia kwenye kasi ya viwango yakinifu
na weledi.
Mhe Mwanjelwa alisema kuwa Wakuu hao wa Idara na
Vitengo wanajukumu kubwa la uwakilishi wa watumishi wenzao 1828 wanaohudumu katika
Wizara ya kilimo kote nchini hivyo ili kuwafanya wananchi kubadili mbinu za
kilimo kutoka kilimo kwa ajili ya chakula pekee hadi kufikia kilimo kwa ajili
ya chakula na biashara ni lazima watumishi wote kuwa wabunifu na kutumia
taaluma zao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Katika kikao hicho kilichoongozwa na Naibu Waziri
Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa Kilihudhuriwa na Mkuu wa Idara ya Utawala na
Rasilimali watu, Sera na Mipango, Mafunzo, Zana za kilimo, Utafiti na
Maendeleo, Usalama wa Chakula, Maendeleo ya mazao na Matumizi bora ya Ardhi.
Wengine ni Wakuu wa Vitengo; Kitengo cha Fedha na
Uhasibu, Kitengo cha Ukaguzi wa ndani, Kitengo cha Habari na Mawasiliano
serikalini, Kitengo cha sheria, Kitengo cha Ugunduzi na Ugavi na Kitengo cha
TEHAMA.
“Kubwa na la msingi ambalo ningependa kuwaasa na
ninyi kukumbuka kuwa hii ni awamu ya tano
ya kazi na mchakamchaka, hivyo badilisheni Mindset ili tufanye kazi kwa
kumsaidia Rais kwa weledi, ubunifu, Maarifa, Juhudi na uzalendo, bado kuna watu
wanatembea badala ya kukimbia’’
“Ni lazima tukimbie lakini uwe mchakamchaka with
Quality kwani watu wanaamini katika matokeo chanya, kwahiyo kuanzia sasa ni
lazima tukimbizane na kasi ya awamu ya tano kwa kuongeza ufanisi kwenye wizara
ya kilimo na business As Usual ni Marufuku” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Mhe Naibu Waziri Dkt Mwanjelwa alisema kuwa
wataalamu wanapaswa kutumia utaalamu wao na kuonyesha matokeo chanya kwani
kufanya hivyo kutaongeza imani kubwa kwa serikali inayotekeleza ilani ya ushindi
ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Aliongeza kuwa Kilimo ni uti wa mgongo kwani zaidi
ya asilimia 75 ya wananchi ni wakulima ambapo mtaji wake ni nguvu na ardhi hivyo
wasiposaidiwa kuboresha kilimo chao na kuongeza uzalishaji ni wazi kuwa Taifa
litaendelea kusalia nyuma kimaendeleo.
Sambamba na hayo pia ameagiza Kuandaliwa Maelezo mafupi (Profile) na Muundo Mpya wa Wizara ya kilimo ndani ya wiki mbili baada ya Wizara hiyo kutenganishwa na Uvuvi pamoja na Mifugo.
Sambamba na hayo pia ameagiza Kuandaliwa Maelezo mafupi (Profile) na Muundo Mpya wa Wizara ya kilimo ndani ya wiki mbili baada ya Wizara hiyo kutenganishwa na Uvuvi pamoja na Mifugo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment