Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi amefanya mkutano Kuimarisha Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kongwa, Akizungumza na Waandishi wa Habari Ndejembi alisema "Tumefanya Mkutano na Wenyeviti wa Vijiji vyote 87, watendaji wa Vijiji na Kata zote za Wilaya ya Kongwa, pamoja na Jeshi la Polisi wakiongozwa na RPC Muruto kuzungumzia maswala mbali mbali ya ulinzi wa wananchi wa Kongwa.
Sisi kazi tu"
Alisema Mkuu huyo wa Wilaya akiwa anamaanisha Makao Makuu ya Chama na Serikali kuwa Dodoma sio jambo la Kawaida, Watakuja Watu wa Kila Aina na wenye Tabia Tofauti ivo Nilazima Kuimarisha Ulinzi na Usalama katika Wilaya Yetu, Mkoa na Taifa kwa Ujumla.
Kongwa ni Wilaya Moja kati ya Wilaya Saba zinazipatikana Mkoani Dodoma, na Kongwa kama Unatoka Dar es salaam basi ndio wilaya yakwanza Kufika kabla yakufika Chamwino na Kisha Dodoma mjini Manispaa.
0 comments:
Post a Comment