11 Oktoba, 2017
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Ndg. Humphrey Polepole leo amekutana na Vijana wa kike wanaojulikana kwa jina la NGUVU YA MWANAMKE na kusisitiza umuhimu wa kuthamini na kutambua nafasi ya mtoto wa kike katika jamii.
Katika siku hii ya kusherekea siku ya mtoto wa kike Dunian ambayo huadhimishwa duniani kote kila 11 Oktoba
"Vijana wa Nguvu ya Mwanamke" wametembelea hospitali ya Mnazi Mmoja na kutoa misaada Mbalimbali katika katika wodi ya Wazazi na baadae kutembelea shule ya sekondari ya Zanaki na kutoa zawadi kwa wasichana wenzao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho hayo na baadae kutembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM amewapongeza wasichana hao kwa jambo jema kabisa la Kijamii walilofanya hasa kutembelea watu wanaokabiliwa na changamoto mbali mbali na kuwapatia hamasa wasichana wenzao.
Ndugu Polepole amesema "Chama Cha Mapinduzi(CCM) kinaamini katika utu nanyi mmefanya jambo jema lenye kuonesha mnajali na kuthamini umoja na mshikamano endeleeni hivyo kwani ndiyo misingi ya chama chetu."
Ndg Polepole amewaambia kuwa nguvu ya Mwanamke iwe chachu ya kuondoa ubifsi na umimi katika jamii zetu lakini kuweni watu wema zaidi katika jamii mnaiyoishi.
Ndugu Polepole amesema mtoto wa kike anauwezo mkubwa kuliko mwanaume ndiyo maana Jamii iliunda mfumo wa kuwagandamiza wanawake.
Amesema wanawake ni watu wavumilivu sana tusiwabeze wanawake kamwe.
Ndugu Katibu mwenezi amesisitiza watoto wakiume waendelee kuelimishwa zaidi ili kuwa na mahusiano mazuri na watoto wa kike ili kujenga umoja na mshikamano baina yao hii itasaidia kuleta usawa katika jamii zetu.
Polepole amesema "kazi ya Mwanamke siyo kuzaa pekee ila wana majukumu makubwa katika Taifa letu zaidi ya hayo mfano kuna wanawake mainjinia, Askari Jeshi, Magereza, Mafundi gereji, Walimu na Viongozi wakubwa".
Uchumi wa Nchi yetu hutegemea kilimo na wanawake ndiyo sehemu kubwa ya Nchi yetu na hujishughulisha na Kilimo. Hivyo tusiwabeze akina mama kote Duniani. Tuwaheshimu kama Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inavyowajali wanawake na imeonesha katika *Ilani ya Ushindi 2015-2020 Fungu la 63*.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) alimaliza kwa kuwaambia Nguvu ya Mwanamke kuwa CCM inaamini kuwa Binadamau wote ni sawa hivyo tuendelee kuwathamini na kuwajali wenye shida na matatizo kama mlivyo fanya leo na mmetenda jambo kubwa na la thamani katika Uhai wenu.
IMETOLEWA NA;
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI.
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
0 comments:
Post a Comment