Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizugumza na wananchi wa Kata ya Ngulyati wilayani
Bariadi katika Mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake yenye lengo la
kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Mchungaji Nicholuos Chimbu mkazi
wa Kijiji cha Ngulyati(kulia) wilayani Bariadi akiwasilisha kero yake
kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) alipofanya
ziara wilayani humo kwa lengo la kuzikiliza kero za wananchi na
kuzitafuatia ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga
wakiteta jambo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa katika Kata ya Ngulyati
aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia
ufumbuzi.
Minza Maduhu mkazi wa Kijiji cha
Ngulyati wilayani Bariadi akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) alipofanya ziara wilayani humo
kwa lengo la kuzikiliza kero za wananchi na kuzitafuatia ufumbuzi
Eliasi Hopi mkazi wa Kijiji cha
Nyasosi Kata ya Ngulyati wilayani Bariadi aliwasilisha kero kwa Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) alipofanya ziara
wilayani humo kwa lengo la kuzikiliza kero za wananchi na kuzitafuatia
ufumbuzi.
Afisa Uhusiano wa TANESCO Mkoa wa
Simiyu akitolea ufafanuzi suala la utekelezaji wa Mradi wa Umeme
Vijijini REA Awamu ya III ambalo liliulizwa na wananchi wa Kata ya
Ngulyati wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka
aliyoifanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia
ufumbuzi.
Kikundi cha Burudani cha Msanii
Polepole kutoka Ngulyati kikitoa burudani ka wananchi na viongozi katika
ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani)
aliyoifanya katika kata ya Ngulyati wilayani Bariadi kwa lengo la
kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony
Mtaka ametoa wito kwa wananchi Wilayani Bariadi mkoani humo kujiunga na
Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF).
Mtaka ametoa wito huo wakati
alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngulyati wilayani Bariadi
wakati wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za
wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Amesema azma ya Serikali ni
kuwa ifikapo mwaka 2020 Watanzania wote wawe wamejiunga na Mfuko wa Afya
ya Jamii(CHF) au Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), hivyo
akawahamasisha wananchi ambao bado hawajajiunga na CHF kujiunga kwa kuwa
gharama yake ni nafuu.
“Watu wa Ngulyati ni
wafanyabiashara wazuri, wafanyakazi wazuri, wakulima wazuri ningetamani
kuwaona wote hapa mnakuwa na kadi za Mfuko wa Afya ya Jamii ambazo
zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000, hii ni sawa na kuku mmoja
tu mnapata matibabu watu sita kwa maana ya baba, mama na watoto wa nne”
amesema.
Ameongeza kuwa Serikali inaendelea
kuimarisha vituo vya kutolea huduma za afya ili wananchi waweze kupata
huduma bora, ambapo Serikali kupitia Mradi wa RBF(Result Based
Financing/Kulipa kulingana na Matokeo) imetoa fedha kwa ajili ya
kuboresha huduma.
Akitoa ufafanuzi wa fedha hizo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bariadi, Ndg.Abdallah Malela
amesema, kupitia mradi wa RBF Halmashauri hiyo imepokea shilingi milioni
260, zilizogawanywa katika vituo vilivyopo 26 vya kutolea huduma za
afya ambapo kila kituo kimepokea shilingi Milioni 10 ili kuboresha
utoaji wa huduma za Afya.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga kufuatilia na
kuhakikisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi anawasilisha
kwake taarifa ya fedha za Mradi wa RBF alizopokea na kazi zilizofanyika
katika vituo vya kutolea huduma.
“Mhe. DC umesikia hapa hawa watu
wamepokea fedha toka mwezi saba mwaka huu na leo ndio wamekaa kikao cha
mpango, maana yake ni kwamba mwezi wa nane wananchi hawajapata huduma
zilizokusudiwa na Wizara ya Afya, na naamini yanayofanyika kwenye kituo
hiki yapo katika vituo vyako vyote, sasa nimuombe Mkurugenzi wa Mji
Jumatatu atuletee taarifa ya mpango uliotekelezeka” amesema Mtaka.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Mhe.Festo Kiswaga amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuwa
atalifuatilia suala hilo pamoja na kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa
katika ziara hiyo na ameahidi kuwachukulia hatua watumishi
watakaoshindwa kutimiza wajibu wao katika kuwahudumia wananchi.
Kuhusu suala la taratibu za
uwekaji wa umeme wa REA awamu ya III kwa wananchi na Taasisi za Umma
ambalo liliwasilishwa na wananchi akiwemo Mwl. Daudi Jackson, Mkuu wa
Mkoa, Mhe.Anthony Mtaka amesema atakutana na Meneja wa TANESCO Mkoa siku
ya Jumatatu Septemba 04, ili wajadili namna na kushughulikia suala
hilo.
Katika hatua nyingine Mtaka
amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
kuhakikisha Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri anafika eneo la ujenzi wa
Soko la Ngulyati Jumatatu tarehe 04 Septemba kukutana na viongozi wa
Kijiji na Kata, kwa ajili ya kuanza mpango wa ujenzi wa soko hilo ili
kutatua kero ya ukosefu wa soko na kuwawezesha wananchi kupata sehemu ya
kuuzia bidhaa zao.
Wakati huo huo Mtaka amewataka
wananchi kutumia vizuri msimu wa kilimo, kulima mazao yanayostahimili
ukame na akawasisitiza kutunza chakula walichokipata katika msimu
uliopita kwasababu Serikali haitakuwa na chakula cha msaada.
0 comments:
Post a Comment