Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelezo ya shule
ya wasichana Dakawa kutoka kwa Makamu Mkuu wa shule hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua miundombinu ya Shule ya sekondari ya wasichana Dakawa.
Wanafunzi
wa shule ya wasichana Dakawa wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri
Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipokuwa akizungumza nao.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua miundombinu ya Shule ya sekondari ya wasichana Dakawa.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na baadhi ya walimu
wa shule ya sekondari ya wasichana Dakawa wakati akifanya ukaguzi wa
majengo ya shule hiyo.
WANAFUNZI
wa kidato cha sita katika sekondari ya wasichana Dakawa iliyopo mkoani
Morogoro wamepania kuwashangaza watanzania katika matokeo ya mwaka ujao
ya kidato cha sita kwa kuifanya shule hiyo kwa miongoni kwa shule 20
bora kitaifa baada ya matokeo yao.
Wasichana
hao wametoa kauli hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tamisemi Mhe. Selemani Saidi Jafo alipofanya ziara ya kushtukiza shuleni
hapo ili kujionea mazingira halisi ya kufundishia na kujifunzia.
Shule hiyo kwa mwaka huu ilikuwa katika nafasi ya 69 kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita.
Kutokana
na hali hiyo, Naibu Waziri huyo aliamua kufanya ziara hiyo kushtukiza
ili aweze kubaini kama kuna changamoto kubwa zinazo wakabili wanafunzi
katika shule hiyo kwa kuwa ni shule ya wasichana pekee.
“Nimeona
nije kujionea mwenyewe kama mambo mazito yana wakwaza ambayo yanaweza
kumkwamisha mtoto wa kike asipate elimu inayo tarajiwa,”amesema Jafo
Katika ziara hiyo, Jafo alifanya ukaguzi wa madarasa, mabweni, nyumba za walimu, jiko, vyoo, maktaba, na bwalo la Chakula.
Jafo
aliwaambia walimu na wanafunzi kwamba serikali ipo katika mpango
kabambe wa shule zote kongwe hapa nchini ili ziwe na mazingira mazuri ya
utoaji wa elimu bora hapa nchini.
Aidha
Naibu Waziri huyo ameonesha kufurahishwa na suala la utunzaji wa
mazingira ya shule ambapo wanafunzi na maeneo yote ya shule ni safi na
yanavutia.
Naibu
Waziri Jafo anaendelea na ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya
barabara, afya, Elimu, Maji na kuzungumza na watumishi katika mikoa ya
Dar es salaam, Pwani, Songwe na Tabora.
0 comments:
Post a Comment