Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi,Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu Mh.Anthony Mavunde jana alikuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi rasmi msimu wa FURSA 2017 mkoani Arusha.
“Tumehutubia sana,tumesema sana, tumejadili sana,tumepanga mipango
sana, sasa ni wakati wa kuachana na dhana hii na kutenda, kufanya, na
sio kufanya tu bali kufanya kweli”.
Ni maneno alionena kwa hisia kali Naibu Waziri Anthony Mavunde akizungumza na mamia ya vijana na vikundi mbalimbali mkoani Arusha Tanzania katika muendelezo wa msimu wa FURSA 2017.
Naibu Waziri Mavunde aliwataka Vijana kuhakikisha wanatumia fursa ya
Mifuko 19 ya Uwezeshwaji Wananchi Kiuchumi kama sehemu ya kupatia mitaji
ya shughuli mbalimbali za kiuchumi na hivyo kusaidia kuondokana na
masharti magumu ya Taasisi za Fedha nyingi.
Aidha pia, Aliwashukuru sana timu nzima ya Fursa chini ya muasisi
ndg.Ruge Mutahaba kwa kuzidi kuisaidia jamii ya kitanzania na serikali
kwa ujumla wake kufanikisha maendeleo ya nchi hii na kuonesha kwa
vitendo dhana nzima ya ushirikishwaji.
Mgeni Rasmi ndugu Mavunde aliizungumzia dhana hii ya Fursa na kauli
mbiu yake mwaka huu ya Anzia Sokoni akiwataka vijana na watanzania wote
wanaotaka kufanikiwa kutokata tamaa na kuwa na malengo yenye tija,
kuhakikisha kila siku wanaitumia kuwaza jambo la kufanya na la kuwaletea
maendeleo.
Pia,alizungumza ni namna gani serikali mpaka sasa imefanya katika
kuhakikisha ina watengenezea vijana mazingira bora na kukazania kwenye
mipango iliyopo kwao kuanzia wale walio katika mfumo rasmi wa elimu na
wale walionje ya mfumo kuwatengenezea mazingira ya kuendeleza shughuli
zao mfano useremala,ushonaji nk kuwapa mafunzo na kuwatengeneza kua
bora.
Mwisho aliwashukuru washriki wa Fursa 2017 Umoja wa mataifa kwa
kuendelea kushika ajenda hii ya vijana ikiwa kwa mkoa wa Arusha kupitia
ILO wanaendelea kutoa mafunzo ya uanagenzi kwa vijana,pia Letshego
Tanzania kwa kujidhatiti kuwasaidia vijana kwa mikopo na sapoti nafuu
pia ushauri katika safari yao ya kujikwamua kimaisha,wadau wengine ni
wazara ya Afya na kampeni yao ya NIPO TAYARI wakihimiza usafi hasa wa
maliwatoni kunawa mikono.
Kuelekea kuhitimisha Mh Mavunde alikubaliana na mtazamo wa FURSA 2017
wa Anzia Sokoni akithibitisha kua katika lolote lile lazima kujua soko
linataka nini.
0 comments:
Post a Comment