Neno La Wakati Mwema
Na Mathias Canal
Ilikuwa ijumaa usiku Agosti 11, 2017 ambapo Tume ya Taifa ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya, IEBC
ilimtangaza Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee kuwa mshindi wa
uchaguzi wa Urais uliofanyika Jumanne Agosti 8, 2017 kuwa ushindi wake uliakisi kura
8, 203, 290 ambazo ni asilimia 54.27 alizopata ukilinganisha na mpinzani wake mkuu, mgombea wa
muungano wa vyama vya upinzani wa National Super Alliance (NASA) Raila Odinga aliyetajwa kupata
kura milioni 6,762,224 ambayo ni asilimia 44.74. Kenyatta alikuwa anawania muhula wa pili baada ya kumshinda Odinga kwenye uchaguzi wa mwaka wa 2013
Nitakukumbusha kwa uchache wakati Akizungumza kwenye hafla ya kutangaza matokeo iliyofanyika katika ukumbi wa Bomas of
Kenya, Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati alisema uchaguzi wa
mwaka huu nchini humo ulifanikiwa na kutekelezwa kwa njia ya ustadi mkubwa tena ukiwa huru na haki.
Mara baada ya matokeo hayo kutangazwa Muungano wa National Super Alliance (Nasa) chini ya Muwania Urais Raila Odinga kwa kauli moja walikubaliana kususia hafla hiyo baada
ya kuwasilisha malalamiko kwa tume hiyo kwamba uchaguzi huo uligubikwa
na dosari japo hata hivyo Haikujulikana mara moja ni hatua gani Odinga na viongozi wengine wa NASA walinuia kuchukua baada ya tangazo hilo.
Katika ukimya huo huo uliwafanya NASA kuibukia mahakamani kufungua Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Urais ambapo kwa siku takribani tano hivi kesi ilianza kusikilizwa katika mahakama ya juu zaidi ya taifa
hilo, huku mahakama hiyo ilipokea malalamiko ya mawakili upande wa upinzani NASA
kwamba Tume ya uchaguzi (IEBC) ilikataa kuwapatia wataalamu wake wa
teknolojia ya mawasiliano fursa ya kuchunguza mitambo ya data ya Tume
hiyo ilizotumiwa kuhesabu kura za Urais, kama ilivyoagizwa na mahakama.
Nitapendelea zaidi kukukumbusha kuwa Muungano huo wa vyama vya Upinzania nchini Kenya NASA ulifungua kesi kwa madai kuwa mitambo ya IEBC iliingiliwa ili kumpatia ushindi Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, tuhuma ambazo tume hiyo ilikanusha vikali.
Nitapendelea zaidi kukukumbusha kuwa Muungano huo wa vyama vya Upinzania nchini Kenya NASA ulifungua kesi kwa madai kuwa mitambo ya IEBC iliingiliwa ili kumpatia ushindi Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, tuhuma ambazo tume hiyo ilikanusha vikali.
Usikilizwaji wa malalamiko uliendelea mahakamani na hatimaye Mahakama ya Juu nchini Kenya
kupitia Jaji David Maraga na wenzake wanne kubatilisha uchaguzi wa Urais wa mwezi Agosti na kuagiza uchaguzi mpya ufanyike katika kipindi cha siku 60. Sababu waliyoisema ya kufuta uchaguzi huo wa Rais Majaji wa mahakama hiyo walisema uchaguzi huo ulijaa kasoro nyingi ambazo ziliathiri matokeo hayo sambamba na uchaguzi kuandaliwa pasina kufuata katiba na sheria za uchaguzi
Hata hivyo wakati usikilizwaji wa kesi ukiendelea Rais Uhuru Kenyatta alisikika kupitia vyombo vya habari akisema kuwa ataheshimu uamuzi
wa mahakama ijapokuwa alihoji ni kwa nini watu sita wanaweza kutoa
uamuzi unaokwenda kinyume na matakwa ya Wakenya. Hata hivyo baadaye alisema kuwa majaji hao walikuwa wamelipwa na ''watu wa kigeni pamoja na wajinga wengine'', huku akisisitiza kuwa 'Maraga
na wahahalifu wake wameamua kubatilisha uchaguzi wote ni Wakora.
Uhuru alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa "Sasa mimi sio tena Rais mteuliwa bali Rais aliye mamlakani. Maraga anapaswa kujua kwamba
sasa mimi ni Rais anayehudumu'' lakini Licha ya vitisho hivyo Rais
Kenyata hana uwezo wa kumfuta kazi jaji mkuu ambaye muhula wake mmoja
unakamilika wakati atakapofikisha miaka 70.
Ndugu zangu ni wazi kuwa Uamuzi wa kufutwa matokeo ya uchaguzi wa Urais nchini Kenya umeifanya nchi hiyo kuwa nchi ya kwanza Afrika ambapo
upinzani umewasilisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Urais na
wakafanikiwa.
Lakini sio sehemu ya kuhalalisha kuwa Kenyata amekuza Demokrasia nchini humo, Maamuzi hayo ya mahakama yamechagizwa na kuwekwa misingi mizuri ya mahakama kufanya maamuzi pasina kuingiliwa kwa namna yoyote ile nikiwa na maana kuwa uzuri wa Demokrasia nchini Kenya umeakisiwa na Katiba kuwa na misingi mizuri.
Ndugu zangu Uhuru Kenyata hawezi kuwa shujaa katika jambo hilo kwa kuwa kenyata na hata Rais mwingine yoyote atakayeshika hatamu nchini Kenya
hawawezi kuwa na mamlaka mengine ya kufanya zaidi ya kuzingatia katiba iliyopo.
Katiba ya Kenya imetoa nguvu za kisheria katika mihimili mingine ya vyombo vya dola hivyo Kenyata hana nguvu ya kufanya jambo lolote katika hilo japo kutokujua na kutokuwa wafuatiliaji wa mambo wapo watu watasema Demokrasia imekuzwa na Uhuru Kenyata, huo ni uvivu wa kufikiri.
Hata hivyo katiba imeondoa nguvu ya Rais katika maamuzi mengi makubwa tofauti na
katiba nyingi za Afrika, binafsi nadhani ingefaa zaidi kama Mgombea Urais wa Muungano wa upinzani nchini Kenya National Super
Alliance (NASA), Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga angepongezwa kwa kuifahamu vizuri katiba na kufanya maamuzi ya kutafuta haki kwa njia ya kisheria kwa kuwasilisha kesi ya kupinga matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi.
kama Katika kipindi cha utawala wa Rais Uhuru Kenyata angekuwa ndiye amebadili katiba na kuondoa nguvu nyingi katika mamlaka yake huenda ingekuwa sehemu ya kuchagiza mjadala kwa kumuunga mkono lakini sivyo, sasa iweje apewe sifa lukuki asizostahili.
Yapo mambo 10 ya kufurahisha na pengine ya kushangaza ulimwenguni ya kujiuliza ambayo watu wengi wamehoji akiwemo Magoiga SN
i) Ni ushahidi kuwa kura zilizompa Uhuru ushindi hazikuwa kura
halali kwa mujibu wa shutuma zilizowasilishwa na NASA. Raila alisema
kuwa Uhuru alikuwa akiongezewa kura kupitia mfumo wa kompyuta
ulioingiliwa. Huu ni wizi na wizi si jambo la kuungwa mkono.
ii) Ni ushahidi kwamba matokeo ya uchaguzi ambayo
baadhi ya watu walikuwa wakiyashabikia na kujivunia hayakuwa matokeo
halali (bali ya wizi. Nadhani wakati wa kuripoti matokeo yaliyokuwa
yakitangazwa na tume ya uchaguzi, kuna watu walikuwa wakiruka kwa vifijo
huku wakijitapa kuwa hawakamatiki kwa jinsi matokeo yanavyoashiria
ushindi (sasa ndiyo inajulikana kuwa hayakuwa matokeo halali, kwahiyo
hata vile vigelegele na tambo za hapa na pale hazikustahili kuwepo)
iii) Ni ushahidi kuwa uchaguzi mliokuwa mkiuita uchaguzi wa huru, haki
na safi haikuwa kweli. Maana maafisa wa tume waliouliwa ndiyo mwanya huo
huo uliotumika kucheza na matokeo na hata kubadilisha matokeo kwa
kutumia ujanja wa kuhadaa mifumo ya kompyuta
iv) Ni ushahidi
kuwa, sababu za kitoto zilizowahi kutolewa na baadhi ya watoto kuwa
Raila Odinga ameshindwa kwa sababu ni rafiki wa Rais wa Tanzania Mhe Magufuli ni uongo maana
mahakama imesema vinginevyo, kwamba Uhuru alishinda kwasababu sheria,
katiba na kanuni za uchaguzi hazikufuatwa na kwamba uchaguzi huo haukuwa
huru na haki pia mahakama imeongeza kuwa matokeo ya uchaguzi huo
yalikuwa batili na yasiyopaswa kutambuliwa.
v) Ni ushahidi kwamba
Raila hakushindwa kwasababu alisema ataongoza Kenya kupambana na
ufisadi kama Mhe Rais Dkt Magufuli anavyofanya Tanzania kama baadhi ya watoto
walivyokuwa wakisema, hata akishindwa mara ya pili haitakuwa sababu ya
kusema ataongoza Kenya kupambana na ufisadi kama Magufuli anavyoongoza
Tanzania.
vi) Ni ushahidi kuwa ushabiki umetawala uwezo wa baadhi ya watu kutafakari mambo, mpaka kusema kuwa Uhuru ameshinda kwasababu ya Lowasa.
Hapana akishinda ni kwasababu ya wakenya kuamua, au 'vifaranga wa
kompyuta' kumsaidia kama alivyotaka kufanya na siyo ushabiki.
vii)
Inatoa tafsiri kuwa kifo cha yule afisa wa tume aliyekuwa akihusika na
mifumo ya kielektroniki hususani ktk kuthibitisha na kuruhusu matokeo ya Urais kinahusika na tuhuma zilizotolewa na NASA kuwa kuna wajanja
waliingilia (hacking) mifumo ya kompyuta na kumuongezea Uhuru kura.
viii) Inatoa tafsiri kuwa kama walijaribu kujiongezea kura kiujanja
janja, na ni tafsiri kuwa hakukuwa na demokrasia ya kweli ndiyo maana
mahakama imebatilisha hayo matokeo. Swali, je kama waliaribu kuiba
mwanzo, hawatajaribu tena kwa kutumia mbinu nyingine mbalimbali mpaka
lengo lao la mwanzo litimie!?
ix) Inatoa tafsiri kuwa,ile tume
ya uchaguzi ya Kenya ambayo watoto wengi wa Tanzania walikuwa wakiitolea
mfano kuwa ni huru na haki kumbe haikuwa huru wala haki bali ilikuwa Tume ya
Uhuru. Mpaka sasa hivi Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi (IEBC) amegoma
kujiuzulu. Je inastahili kuendelea na uchaguzi wa marudio, au
ibadilishwe ??
x)Inatoa tafsiri kuwa huenda Waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa kutoka Umoja wa Ulaya (EU), Umoja wa
Afrika (AU), Marekani na Jumuiya ya Madola na Jumuiya ya Afrika huwa ni watalii, maana walisema shughuli ya upigaji kura iliendeshwa kwa njia huru na
haki na kwa njia ya amani
ilihali mahakama ya juu imesema kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki na
wala haukufuata sheria na katiba. Kuna haja ya kuendelea kuwaamini hawa
waangalizi wa kimataifa?
HITIMISHO
Nisikia Naibu Rais wa Kenya , William Ruto, akiiambia Tume ya uchaguzi ya Kenya
kutaja rasmi siku ya kurudiwa kwa uchaguzi wa Urais nchini humo yaani amesahau kabisa kwamba Mahakama alisema uchaguzi urudiwe ndani ya siku 60 tangu kufutwa kwa uchaguzi kwahiyo hata hesabu ya kutambua ni lini siku 60 zinafika ukomo kwa Ruto imeshindikana kweli wizi haujawahi kumuacha mtu salama inapelekea kupoteza kumbukumbu.
Katika kipindi hiki nilitegemea zaidi Rais Uhuru Kenyata angekuwa mtulivu zaidi kuliko vitisho alivyoanza kuvitoa kwa Mahakama na majaji waliobatilisha ushindi wake ambao ulikuwa unabaka Demokrasia.
Zaidi nilitegemea Rais Uhuru Kenyata kutangaza kujiuzulu nafasi ya urais ama hata kutogombea tena Urais kutokana na kukutwa na ushindi usiokuwa halali kwa njia ya udanganyifu lakini pia nilitegemea wote waliohusishwa na udanganyifu huo kujiuzulu, kufutwa kazi na
hata kuchukuliwa hatua za kisheria kwani kamwe hawawezi kuaminiwa
kusimamia uchaguzi ujao.
Mwisho, Mgombea wa Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya wa National Super Alliance (NASA) Raila Odinga kwa uamuzi wake wa budara wa kufuata haki yake kupitia vyombo vya sheria tofauti kabisa na wengine ambao hutaka haki zao kupitia Operesheni UKUTA, Nimpongeze Jaji wa mahakama ya juu kabisa nchini Kenya Jaji David Maraga na wenzake wanne kubatilisha uchaguzi wa Urais kutokana na kubaini kasoro nyingi hili limekuwa fundisho pia kwa wafuasi wengi nchini Tanzania waliokuwa wanapigia chepuo kukua kwa Demokrasia ya wizi wa kura nchini Kenya.
Ni Neno La Wakati Mwema
Mathias Canal
0756413465
Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment