Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akikagua uwanja wa
Machinga uliopo mjini Tukuyu ambao umebadilishwa matumizi na Halmashauri
ya Rungwe kwa kukosa sifa w badala yake uwanja wa michezo sasa utakuwa
unatumika ule wa Tandale mjini humo.
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akiongea na wananchi na
wanamichezo (hawapo pichani) waliokuwa wanashiriki Tamasha la Ngoma za
Jadi linaloratibiwa na Taasisis ya Tulia Trust mjini Tukuyu
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (wa pili kushoto)
na Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson
wakibeba nyoka anyetumiwa kwa kucheza ngoma ya Bogobogobo kutoka Bujora
Mwanza. (Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Tukuyu)
………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi, Tukuyu, Mbeya
Halmashauri ya Rungwe
imebadilisha matumizi ya uwanja wa zamani wa mpira wa miguu uliopo mjini
Tukuyu unaojulikana kama machinga kuendelea kutumika kwa matumizi
mengine kutokana na kukosa sifa za uwanja huo kukosa sifa.
Badala yake Halmashauri hiyo
imetoa uwanja wa Tandale uliopo mjini Tukuyu kutumika kwa michezo
mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu na matamasha mbalimbali.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya
ya Tukuyu Bw. Julius Chalya alipokuwa akitoa taarifa fupi ya shughuli za
maendeleo katika wilaya hiyo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Anastazia Wambura alipokuwa katika ziara ya kikazi
mkoani Mbeya.
“Uwanja wa mwanzo unaojulikana
kama uwanja wa Machinga uliokuwa unatumika kwa michezo kwa sasa haufai
kwa matumizi ya michezo kwa kukosa sifa, hivyo halmashauri imebadilisha
matumizi yake ili uendelee kutumika kwa matumizi mengine ikiwemo kituo
cha mabasi yanayotoa huduma katika halmashauri na bishashara nyingine”
alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Akizungumzia kuhusu uamuzi wa
halmashauri wa kubadilisha matumizi ya uwanja huo wakati wa kufunga
Tamasha la pili la Ngoma za Asili linaloendeshwa na Taasisi ya Tulia
Trust, Naibu Waziri Wambura amesema kuwa Serikali inaendelea kusisitiza
halmashauri ziendelee kutenga maeneo yanayofaa kwa michezo kwa kutimiza
vigezo vinavyotakiwa kwa ajili ya michezo.
Uwanja wa Tukuyu uliokuwa
unatumika zamani kwa michezo umekosa vigezo vya kuendelea kutumika kama
uwanja wa michezo kutokana na vipimo vyake kuonesha kuwa ni mdogo kwa
kiwango cha halisi unatakiwa kuwa na urefu wa mita 68 na huo wa Tukuyu
una mita 44.
Kuhusu kuendeleza kiwanja cha
Tandale ambao umetolewa na halmashauri kwa ajili ya michezo, Naibu
Waziri Wambura ameliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupitia
Katibu Mtendaji wake Mohamed Kiganja kushirikiana na halmashauri hiyo
kwa kutoa ushauri wa kitaalamu kuendeleza uwanja huo ili wananchi wa
Rungwe waweze kuutumia kuboresha afya zao kwa kufanya mazoezi pamoja
kunufaika na fursa za kiuchumi wakati wa mashindano mbalilmbali
yatakayofanyika uwanjani hapo.
Kupatikana kwa uwanja wa Tandale
utnaotumika kwa sasa kwa michezo mbalimbali mjini Tukuyu kumepokelwa na
kwa furaha na wananchi waliofurika viwanja hivyo wakati wa kuhitimisha
Tamamsha la pili la Ngoma za Jadi linaloratibiwa na Taasisi ya Tulia
Trust ambapo mwasisi wake Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ameanza kampeni ya kuirudisha timu ya Tukuyu Stars kwa kuwahamasisha
Wabunge wa mkoa wa Mbeya na wananchi kuiwezesha timu hiyo kurudi Ligi
Kuu ya Tanzania ya Vodacom.
0 comments:
Post a Comment