Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi
Evarist Ndikilo ,akifungua mafunzo ya siku tano ya wadadisi wa utafiti
wa kilimo mwaka 2016/2017 ,yaliyoandaliwa na ofisi ya takwimu taifa
(NBS). Picha na Mwamvua Mwinyi
………………
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
SERIKALI mkoani Pwani,imetoa rai
kwa watendaji ,wenyeviti wa mitaa/vijiji na wataalamu kuhakikisha
wanashirikiana na wadadisi na wasimamizi watakaofanya kazi ya utafiti wa
kilimo mwaka 2016/2017,ili kupata takwimu halisi .
Hatua hiyo itasaidia ,kupanga
mipango ya maendeleo katika sekta ya kilimo ambayo inaajiri zaidi ya
asilimia 75 ya watanzania hasa katika maeneo ya vijijini.
Akifungua mafunzo ya siku tano ya
wadadisi wa utafiti wa kilimo mwaka huu wa fedha,mkuu wa mkoa wa Pwani
mhandisi Evarist Ndikilo,alisisitiza endapo utakuwepo ushirikiano mzuri
utawezesha kuweka mikakati ya baadae ya kimkoa na taifa.
Aidha aliwaomba wananchi kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa wadadisi na wasimamizi hao ili kutoa taarifa
sahihi kuhusiana na utafiti.
Mhandisi Ndikilo,alieleza kwa
mujibu wa sheria ya takwimu namba 9 ya mwaka 2015 taarifa
zitakazokusanywa zitatunzwa kwa usiri na zitatumika kusimamia kupatikana
takwimu halisi za kilimo.
Alisema,sekta ya kilimo ina
mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi ambapo mwaka 2016 mchango wa sekta
hiyo pato la taifa ulikuwa asimilia 29.1
”kati ya asilimia hiyo kilimo cha
mazao kilichangia asilimia 15.5,“Mifugo asilimia 7.7 ,misitu asilimia
3.9 na sekta ya uvuvi ilichangia asilimia 2.0 “alisema mhandisi Ndikilo.
Mkuu huyo wa mkoa alisema,mafunzo hayo ni hatua muhimu katika,utekelezaji wa mipango ya kuboresha maisha ya watanzania.
Mhandisi Ndikilo,alifafanua
serikali imeandaa mipango madhubuti ya muda mfupi na mrefu inayolenga
katika kuimarisha uchumi na kuondoa umaskini ikiwa ni pamoja na dira ya
taifa ya maendel;eo ya mwaka 2025 .
Alisema ,hivyo serikali na wadau
bado inaendelea kuhitaji takwimu rasmi kwa ajili ya kupanga utekelezaji
na kutathmini program mbalimbali za maendeleo ya kitaifa ,kikanda na
kimataifa .
Dira ya taifa ya maendeleo ya
mwaka 2025 na mpango wa pili wa taifa wa maendeleo wa miaka mitano
unaoanza kutekelezwa mwaka huu wa fedha.
Mhandisi Ndikilo,alibainisha
kuwa,baada ya kukamilika kwa utekelezaji wa malengo ya millennia ya
mwaka 2015 Tanzania na dunia kwa ujumla.
Aliishukuru serikali ya Marekani
kupitia shiriki lake la mendeleo ya kitaifa USAID kwa msaada wa kiufundi
na fedha uliowezesha kufanikisha utafiti .
Mtakwimu kutoka ofisi ya takwimu
taifa (NBS),ambae pia ni mratibu wa mafunzo hayo kanda ya Mashariki,
Theresia Sagamilwa,alisema mafunzo yanafanyika kikanda ,ambapo kanda
hiyo inahusisha mkoa wa Pwani,Lindi,Mtwara na Dar es salaam.
Alisema lengo kuu la mafunzo hayo ,ni kukusanya taarifa za uzalishaji kwa kilimo na ufugaji kwa mwaka wa kilimo uliopita.
Theresia alieleza,utafiti
unafanyika nchi nzima ,”na wanaomaliza mafunzo ya udadisi wataenda
kwenye mikoa yao uhusika kuendelea na zoezi la utafiti.
Mdadisi kutoka Lindi,Makenza
Matola alishukuru kupatiwa mafunzo ambayo yatawasaidia kufanya zoezi la
udadisi kwa kina na kujua uzalisha wa kilimo kwa kipindi kilichopita.
Sensa ya kilimo huwa ikifanyika
baada ya miaka kumi lakini kwa sasa imerahisishwa ambapo kunafanyika
utafiti wa kilimo na mifugo kila mwaka.
0 comments:
Post a Comment