Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefunguka na kusema kuwa
mtu yoyote akifanya makosa ya nchi nzima atachukuliwa na kupelekwa
sehemu yoyote ambapo mamlaka zinazofanya jambo hilo zitaona panafaa.
Mwingulu
Nchemba amesema hayo jana wakati akijibu swali la Mbunge Dkt. Suleman
ambaye alihoji uhalali wa baadhi ya Masheikh kuhamishwa kutoka Zanzibar
na kuletwa Tanzania Bara kuhukumiwa katika mahakama za Tanzania bara na
kusema ni kinyume na sheria.
"Mhe
Spika spingani na muuliza swali kwenye upande wa vipengele vya sheria
lakini naomba nimwambie tu kwamba kuna makosa ambayo 'specifically' siyo
ya kijiografia mfano watu wakifanya makosa ya kung'oa michikichi Kigoma
hilo unaweza kulitaja ni kosa la Kigoma, kama watu watang'oa karafuu
Pemba ni kosa ambalo unaweza kusema la Pemba.
"....
lakini yanapofanyika makosa ya nchi nzima Mtanzania yoyote au raia
yoyote awe wa Tanzania au nje ya Tanzania atachukuliwa na taratibu za
kufuata haki na sheria zitafanyika pale ambapo mamlaka inayofanya hatua
hizo inaona ndipo panafaa" alisema Mwigulu Nchemba
0 comments:
Post a Comment