Mkurugenzi wa Kiwanda Mtendaji wa
Kiwanda cha Nyuzi Tabora Urveshi Rajani akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa
Tabora Aggrey Mwanri jana mitambo kutengeneza nyunzi wakati
alipotembelea kiwanda hicho kujionea hali ya uzalishaji.
Mitambo ya Kiwanda cha Nyuzi Tabora ambayo hivi sasa haifanyi kazi licha ya kuwa mizima.
Na Mwandishi wetu, Tabora
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri ameteua Mkuu wa Wilaya ya Queen Mlozi kuongoza Kamati
aliyoichagua kwa ajili ya kufuatilia viwanda mbalimbali ili kuangalia
hali halisi na kama vimeshindwa kufanyakazi viweze kupewa Wawekezaji
wengine.
Mwanri aliteua Kamati hiyo jana mjini Tabora wakati wa Mkutano na wadau mbalimbali na Mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi cha Tabora.
Wengine waliochaguliwa ni
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philipo Ntiba ,Afisa
Biashara Mkoa Lucas Kusare ambaye ni Katibu wa Kamati, Mwanasheria wa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Richard Lugomela na Mkuu wa Kitengo cha Habari na
Mawasiliano Serikalini Tiganya Vincent.
Alisema kuwa Kamati hiyo
itaanza na Kiwanda cha Nyuzi Tabora ambapo itaangalia mpango kazi wake ,
itakagua mashine zote kama zinafanyakazi na uwezo wa kifedha wa
mwekezaji huyo kama anao mtaji wa kutosha wa kuendesha kiwanda.
Mambo mengine
yatakayofuatiliwa na Kamati hiyo ni pamoja na kuangalia matatizo ambayo
Mwekezaji huyo aliyaeleza kuwa ukosefu wa soko la nyuzi zake kutokana na
viwanda ambavyo ndio vilikuwa vikinunua kwake kuanza kuagiza toka nje
bidhaa hizo.
Mkuu huyo Mkoa aliongeza kuwa
mambo mengine ambayo Kamati itayafanya ni kuangalia fursa za masoko ya
bidhaa za Kiwanda hicho kama vile Bohari Kuu za Dawa(MSD), Chama Kikuu
cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU) na
wafanyabiashara wengine wanaweza kununua bidhaa zake.
Alisema kuwa Kamati hiyo itatakiwa kila baada ya siku tatu impelekee taarifa ya maendeleo ya kazi yao.
Katika hatua nyingine Mkuu
huyo wa Mkoa ametoa mwezi mmoja kwa Mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora
kuhakikisha mashine zake zinafanyakazi.
Alisema kuwa baada ya kipindi
kuisha atakwenda kukagua na akikuta hakuna kitu atalazimika kumuomba
Waziri wa Viwanda aje kuchukua hatua ikiwemo kumpa mwekezaji mwingine.
Mkuu huyo Mkoa alisema kuwa
hata kama mali ghafi kwa sasa hivi hakuna anataka ni kujiridhisha kuwa
mashine zote ni zima wakati akiwa anasubiri msimu wa pamba ujao ili
apate mali ghafi.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora yuko
katika zoezi la kuhakiki viwanda vyote ili kujiridhisha kama
vinafanyakazi na vile ambavyo wamiliki wake wameshindwa waweze
kuvirudisha Serikalini
0 comments:
Post a Comment