Mtoto
mchanga wa kike anayekadiliwa kuwa na umri wa siku moja ameokotwa
kwenye shimo la choo kinachotumika katika mtaa wa Lumala Kata ya
Kawekamo Wilayani Ilemela mkoani Mwanza akiwa hai baada ya kutupwa na
mzazi wake.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kusema baada ya muda mchache kupita toka kichanga hicho kutupwa
kwenye shimo hilo la choo, polisi walipata taarifa na kwenda kusaidia
kumtoa mtoto huyo ambaye sasa amepelekwa hospitali ya Sekou Toure kwa
matibabu zaidi.
"Inadaiwa
kuwa baada ya muda mchache kupita toka mtoto alipotupwa, palikuwa na
mtu aliyekwenda kujisaidia chooni ndipo akiwa chooni alisikia sauti ya
mtoto mchanga akilia toka ndani ya shimo la choo. Inasemekana kuwa baada
ya mtu huyo kusikia sauti hiyo ya mtoto akilia, alikwenda kutoa taarifa
kwenye uongozi wa serikali za mtaa ambapo uongozi wa mtaa ulifika
mahali hapo kisha ulitoa taarifa kituo cha polisi" alisema Msangi na
kuongeza;
"Askari
baada ya kupokea taarifa hiyo walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo
la tukio na kushirikiana na wananchi waliokuwepo eneo hilo na
kufanikiwa kutoa kichanga hicho cha mtoto toka ndani ya shimo la choo
kikiwa hai. mtoto amepelewa hospitali ya mkoa ya sekou toure kupatiwa
matibabu na hali yake inaendelea vizuri. Polisi wapo katika upelelezi na
msako katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza, ili kuweza kubaini
mzazi/wazazi wa mtoto huyo ambao wamefanya ukatili huo dhidi ya mtoto,
ili baadae waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili hatua stahiki
za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao na iwe fundisho kwa wengine".
Kamanda
Msangi ametoa wito kwa wazazi na walezi kuacha tabia ya kutenda ukatili
dhidi ya watoto ikiwepo vitendo vya kutupa watoto kwani ni kosa la
jinai na endapo mtu atabainika kufanya hivyo hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi yake
0 comments:
Post a Comment