Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amepiga marufuku Halmashauri zote Mkoani
humo kutoza ushuru wa biashara ndogondogo zinazofanywa na wananchi kwa
kutandika na kupanga bidhaa zao chini au kuuzwa katika mabeseni maarufu kama
matandiko.
Mtaka
ametoa agizo hilo baada ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Igaganulwa, Mhe.Nhandi
Masaka Kachala na baadhi ya wananchi kutoa malalamiko yao kuhusu ushuru huo, wakati
wa ziara yake wilayani Bariadi yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na
kuzitafutia ufumbuzi .
Amesema
suala hilo lilishatolewa maelekezo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, hivyo Halmashauri zinapaswa kubuni vyanzo vipya
vya mapato vyenye tija kwa Halmashauri na wananchi badala ya kutegemea kutoza
ushuru unaowakwaza wananchi.
“Kama kuna
Halmashauri bado inatoza ushuru wa matandiko wamechelewa sana, kuanzia kesho
hamna huo ushuru, kama ninyi mnafikiri mapato ni kutoza tandiko la nyanya,
dagaa, mchicha na ninyi kama wakuu wa
idara hiki ndicho chanzo mnachokifikiria kichwani hiyo kazi haiwafai, mkatafute
kazi nyingine ya kufanya” alisema Mtaka.
“Halmashauri lazima ibuni chanzo cha mapato
chenye tija kwenye Halmashauri na watu. Sasa mtu anahangaika na beseni lake la
nyanya wewe unamtoza ushuru, umechangia nini, beseni si lako nyanya si zako” alisema
Mtaka.
Aidha, ameitaka
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
kuhakikisha kuwa inarejesha asilimia Kumi ya mapato yanayokusanywa
inayokusanywa kutoka katika vijiji vyote kwenye kila robo mwaka ili Vijiji
hivyo viweze kutekeleza mipango ya maendeleo iliyowekwa.
Katika hatua
nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewahamasisha wananchi kuendelea kulima pamba kwa
kuwa Serikali imekusudia kujenga kiwanda cha bidhaa ya Afya zitokanazo na zao
la pamba mkoani humo na wataalam wanaofanya upembuzi yakinifu wanatarajia
kufika Mkoani Simiyu Septemba 20 mwaka huu kuja kuona eneo kitakapojengwa
kiwanda.
Amesema wananchi
wasikate tamaa kulima pamba kwa sababu ya matatizo ya kihistoria na kuwaeleza
kuwa, Serikali ya Mkoa imepanga mikakati madhubuti ya kuirudisha pamba kuwa
dhahabu, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata mbegu bora, dawa,
pembejeo zote na suala la bei ya pamba itaanza kujadiliwa mapema.
Ameongeza kuwa
wananchi wasiache kulima mazao jamii ya mikunde hususani choroko na dengu kwa
kuwa Serikali inashughulikia suala la upatikanaji wa soko la uhakiki pamoja na
kupunguza au kuondoa kabisa madalali
katika biashara ya mazao hayo ili wananchi wanufaike kupitia kilimo.
Akitolea
ufafanuzi hoja ya Diwani wa Kata ya Ikungulyabashashi Mhe.Bupi Maduhu Litunga
ya kupimiwa maeneo, Mkuu wa Mkoa huyo wa Mkoa amemuagiza Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya Bariadi kupitia Idara ya Ardhi, kuitisha mikutano katika
Vijiji vyote ambavyo wananchi wanahitaji kupimiwa maeneo na baadae awasilishe
mihutasari ya vikao hivyo Ofisini kwake tarehe 13/09/2017.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amekamilisha ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya
ya Bariadi ambapo amesikiliza na kutatua kero za wananchi katika sekta ya Elimu,Afya,
Kilimo, Mifugo, Ardhi, Ujenzi, Biashara na Uchumi pamoja na suala la utekelezaji
wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA) ambazo amezitolea maelekezo na ameahidi
kufuatilia utekelezaji wake.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kata ya Dutwa(hawapo pichani)
Wilayani Bariadi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha
Igaganulwa wakati wa ziara yake
aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akizungumza
na wananchi wa Kata ya Dutwa (hawapo pichani)katika Mkutano wa Hadhara
uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa
wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka aliyofanya Wilayani humo kwa lengo la kusikiliza kero za
wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Diwani wa Kata ya Dutwa
Wilayani Bariadi, Mhe.Mapolu Nunde Mkingwa akizungumza na wananchi wa Kata hiyo
(hawapo pichani)katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha
Igaganulwa wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka
aliyofanya Wilayani humo kwa
lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wajumbe wa Serikali
ya Kijiji cha Igaganulwa Kata ya Dutwa (hawapo pichani)
Wilayani Bariadi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kijijini hapo
wakati wa ziara yake aliyofanya kwa lengo la
kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Diwani
wa Kata ya Sapiwi, Mhe. James Kibuga Wilayani Bariadi akizungumza na wananchi
wa Kata ya Dutwa (hawapo pichani)katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika
Kijiji cha Igaganulwa wakati wa ziara
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka
aliyofanya Wilayani humo kwa
lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mganga Mkuu wa
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi akifafanua jambo katika Mkutano wa Hadhara
uliofanyika katika Kijiji cha Igaganulwa
wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka aliyofanya
Wilayani humo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia
ufumbuzi.
Kaimu Meneja wa Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) Mkoa wa Simiyu, Jarlath Mushashu akizungumza na
wananchi wa Kata ya Dutwa juu ya umuhimu wa kujiunga na Bima ya Afya na Mfuko
wa Afya ya Jamii wakati wa ziara Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka aliyofanya
Wilayani Bariadi kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia
ufumbuzi.
Baadhi ya Wananchi wa
Kata ya Dutwa wakimsikiliza wilayani Bariadi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji
cha Igaganulwa wakati wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi
na kuzitafutia ufumbuzi.
Mpina Nkwabi Mkazi wa
Dutwa Wilayani Bariadi akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati wa ziara yake wilayani humo yenye
lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthoy Mtaka akiwaonesha Kadi ya matibabu kwa Wazee inayotolewa kwa wazee
wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuwasihi wazee ambao hawajaajiandikisha
wajiandikishe wakati wa ziara yake wilayani Bariadi yenye lengo la kusikiliza kero
za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthoy Mtaka akiwaonesha Kadi ya matibabu kwa Wazee inayotolewa kwa wazee
wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuwasihi wazee ambao hawajaajiandikisha
wajiandikishe wakati wa ziara yake wilayani Bariadi yenye lengo la kusikiliza kero
za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
0 comments:
Post a Comment