Na
Kudra Mawazo, Zanzibar
Kituo
cha huduma za sheria Zanzibar kimetoa mafunzo kwa walimu wa sekondari na msingi
wa somo la uraia kwa lengo la kuwajengea uwezo walimu wa somo hilo, mafunzo hayo
yanatolewa kwa walimu wa shule zilizopo kwenye mikoa yote mitatu ya
unguja.
Kaimu
mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho hicho Ally Haji amesema kuwa kituo kimekuwa
na utaratibu wa kuwapa mafunzo mbalimbali ili kuweza kuwasomesha
wanafunzi na kuwapa mbinu mbali mbali za jinsi ya kuweza kutatua matatizo
yanawakabili.
Alisema
kuwa elimu ya uraia katika jamii inaweza kumuongoza mwanajamii katika ushiriki
wa ulinzi wa taifa lake,kutambua wajibu na haki zao,kuthamini na kutetea katiba
za nchi pamoja na kuelewa misingi ya utawala wa kidemocrasia.
Haji
amewataka walimu hao kuyatumia mafunzo wanayopatiwa kwa lengo la kuwapa
wanafunzi stadi na ufahamu,maadili,maarifa na muelekeo utakaowawezesha
kushiriki katika mambo mbalimbali ya kuijenga nchi yao.
Alisema
kuwa elimu ya uraia ni moja ya njia ya kumfahamisha mwananchi umuhimu wa
kutafuta na kutunza cheti cha kuzaliwa na masuala yanayohusu usajili wa vizazi
na vifo,ufatiliaji wa kitambulisho cha utaifa na kujua umuhimu wa nyaraka hizo
muhimu.
Alisema
kuwa kukosekana kwa elimu ya uraia kwa jamii imepelekea baadhi ya wananchi
kushindwa kujua umuhimu wa vitu hivyo na kushindwa kuvifatilia.
Hata
hivyo Haji alisema ni muda sasa umefika kwa walimu wa somo la uraia
kuwafundisha wanafunzi elimu ya sheria na katiba na ni wajibu wa walimu wa somo
la uraia kuwajibika katika kuwafundisha wanafunzi Kwa ufanisi na weledi kwa
lengo la kupata kizazi kizuri kitakacho kuwa kinafuata kwa vitendo elimu ya
uraia.
0 comments:
Post a Comment