Na Sales Malula
Kanisa la Tanzania Assemblies of God (Victory Christian Centre) Mbezi Beach A Jijini Dar es salaam limeandaa mkutano mkubwa wa uwekezaji. Katika mahojiano maalumu na Mtandao huu Kiongozi wa Kanisa hilo Mchungaji Dk Huruma Nkone amesema maandalizi ya mkutano huo wa wanataaluma yamekamilika na hakutakua na kiingilio chochote.
Dk.Nkone alisema mkutano utafanyika September 10 mwaka huu kuanzia saa kumi hadi saa kuminambili jioni ambapo mkutano huu haubagui dini ya mtu Bali ni ya wananchi wote wenye nia yakuwekeza katika majengo.
Katika mahojiano maalum mnenaji katika mkutano huo Bw.Mchechu amesema amejipanga vyema kuwahudumia watu wote bila kujali madhehebu yao ili kuwapa elimu muhimu itakayowasadia katika maisha yao.Alisema Mungu ndiye mwasisi wa masuala ya uwekezaji huku akinukuu zaburi ya 23 kuwa inaeleza mambo yote muhimu yanayohusu masuala ya uwekezaji huku akitoa wito kwa wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kuja kujifunza somo hili muhimu ambalo litafundishwa bure Kabisa.
0 comments:
Post a Comment