Na Masanja Mabula – Pemba
Katika
mwendelezo wa operasheni wa utokomezaji wa madawa ya kulevya wa Jeshi
la Polisi nchini hatimae Jeshi hilo mkoa wa Kusini Pemba jana
limefanikiwa kumkamata kijana mwengine akiwa na jumla ya kete 241
zinazosadhaniwa kua ni madawa ya kulevya.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi kamanda wa polisi mkoa wa kusini Pemba
Shekhan Mohammed Shekhan amemtaja kijana waliyemkamata kuwa ni Haji
Balozi Hassan (35) ambae alikuwa kwenye gari ya abiria akitokea mkoani
kuelekea micheweni.
Alisema
katika gari hiyo askari walimtilia mashaka abiria huyo ndipo walipoamua
kumpekua na kufanikiwa kumkamata na madawa hayo aliyokua nayo katika
mifuko yake ya suruali.
”
Mpaka hivi sasa yupo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi na leo
tutampeleka mahakamani kusomewa kosa lake” alisema Kamanda Shehan
Kamanda
Shehan ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi ili
kufanikisha kutokomeza madawa ya kulevya yanayoonekana kuwa ni tatizo
katika jamii.
Tukio
la kukamatwa Hassan ni tukio mfululizo wa watuhumiwa wa madawa hayo
kukamatwa kisiwani Pemba ambapo juzi Jeshi hilo lilifanikiwa kumtia
mikononi mwanamke mmoja mkaazi wa Wete akiwa na kete 3621 zinazodhaniwa
kuwa ni madawa ya kulevya katika maeneo ya mbuguani Mkoani.
0 comments:
Post a Comment