Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibaha
Sozi Ngate akitoa hotuba yake katika mahafali hayo ya 12 ya shule ya
msingi Kibaha Independent yaliyofanyika shuleni hapo
Katibu Tawama Wilaya ya Kibaha
Sozi Ngate wa kulia akisalimiana na mmoja wa viongozi wa shule hiyo Said
Mfinanga kushoto katika mara baada ya kumaliza kutoa hotuba yake
katika sherehe za mahafali hayo.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi
Kibaha Independent Charles Majani akitoa maelezo kuhusina na shule hiyo
katika sherehe za mahafali hayo
mmoja wa wanafunzi waliohitimu
darasa la saba katika shule hiyo ya Kibaha Independent akipokea cheti
chake kutoka kwa mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kibaha Sozi Ngate
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la
saba katika shule hiyo ya Kibaha Independent wakionyesha umahiri wake wa
kucheza moja shoo katika mahafali hayo.
PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU
…………………………
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
WANAFUNZI wa shule za msingi ambao
wamemaliza darasa la saba wametakiwa kuachana na vitendo vya kutumia
muda wao kwa kushinda vijiweni na kujiingiza na utumiaji wa madawa ya
kulevya kwani kufanya hivyo kunachangia kwa kiasi kikubwa kunapoteza
nguvu kazi ya Taifa.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kibaha Sozi Ngate ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati
wa sherehe za mahafali ya 12 ya shule ya msingi ya Kibaha Independent
iliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo na kuhudhuliwa na viongozi
mbali mbali wa dini na serikali .
Sozi alisema kwamba kuwa wanafunzi
wa hao ambao wamemaliza darasa la saba kwa sasa wanatakiwa kuzingatia
maadili ambayo wamefundishwa na walimu wao wakati wa kipindi chote
ambapo wakiwa shuleni na kuhakikisha wanaepukana kabisa na tabia ya
kujiingiza katika makundi hayo ambayo hayana faida kwa upande wao.
“Mimi napenda kuwahasa wanafunzi
ambao mmemaliza darasa la saba kuhakikisha kuwa mnazingatia maadili
mazuri ambayo mmefundishwa na walimu wenu, na kwamba vitendo vya
utumiaji wa madawa ya kulevya nisingependa kuona kabisa mnafikia hatua
hiyo kwani kufanya hivyo kunawasababishia madhara makubwa ya kiafya na
kutotimiza malengo yenu,”alisema Sozi.
Pia Sozi aliwataka wazazi na
walezi kuachana kabisa na tabia ya kuwaozesha watoto wao pindi
wanapokuwa masomoni kwani kufanya hivyo kunawanyia haki yao ya msingi ya
kuweza kupata elimu ambayo ndio ufunguo wao wa maisha.
“Kiukweli mimi sipendi kabisa
kuona mzazi au mlezi anaamua kumwezesha mtoto wake na hatimaye
anakatisha masomo, hii kiukweli kwa upande wetu kama serikali hatuwezi
kuivulimia kwani ni kiunyume kabisa na sheria kwa hivyo kitu kikubwa ni
kuhakikisha mnaendelea kuwapatia malezi bora ili waweze kutumiza malengo
yao waliyojiwekea,”alisema Sozi.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa
Kibaha Independent Charles Majani alibainisha kwamba wataendelea
kushirikiana na serikali ya awamu ya tatu katika kuhakikisha wanaboresha
elimu kwa wanafunzi hao ili kuweza kupunguza changamoto mbali mbali
zilizopo katika sekta ya elimu
Alisema kwamba katika shule hiyo
wameweka mikakati ya kuwajengea uwezo wanafunzi wao waweze kujifunza
mambo mbali mbali ambayo yataweza kuwasaidia kufanya vizuri katika
mitihani yao na kutimiza ndoto zao waliojiwekea.
Kadhalika aliiomba serikali
kuhakikisha wanaiboresha zaidi mitaala ya kufundishia kwa lengo la
kuweza kuongeza ufanisi zaidi katika suala zima la kuwafundisha
wanafunzi ili waweze kuelewa zaidi na kufanya vizuri katika masomo yao
na kuongeza kiwango cha ufaulu.
0 comments:
Post a Comment