Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi akifurahia jambo Balozi wa Ireland Nchini Tanzania
Mhe. Paul Sherlock walipokuwa wakiagana nje ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kushoto
kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Mageni Lutambi na wa kwanza
kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo.
Balozi wa Ireland
Nchini Tanzania Mhe. Paul Sherlock leo amefanya ziara mkoani Singida na kuahidi
kuangalia namna ya kufadhili ujenzi wa mabwawa ili yaweze kusaidia kilimo cha
umwagiliaji na sio kutegemea mvua pekee.
Mhe. Sherlock amewatembelea
wanufaika wa misaada wanayotoa katika Vituo vya kulelea watoto wanaoishi katika
mazingira hatarishi vya Siuyu na Faraja, mara baada ya yeye na mabalozi wengine
kumaliza shughuli maalumu bungeni Dodoma.
Ameeleza kuwa
amefurahishwa na hali ya hewa ya Mkoa wa Singida huku akisema kuwa uwepo wa barabara
nzuri umerahisisha safari yake Mkoani hapa ambapo ni jirani na makao makuu ya
nchi.
Mhe. Sherlock
ameongeza kuwa anautazama mkoa wa Singida katika sura ya maendeleo zaidi
kutokana na fursa zilizopo huku akiahidi kuanzisha miradi itakayosaidia
kuongeza mnyororo wa thamani wa zao la alizeti linalozalishwa kwa wingi Singida.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi amesema ameupokea ujio wa balozi huyo kwa furaha
kubwa kwakuwa hiyo ni ishara ya kufunguliwa zaidi kwa milango ya mahusiano
mazuri.
Dkt Nchimbi amesema
moja ya faida ya Singida kuwa jirani na makao makuu ni kupata wageni ambao
wanaitazama Singida kwa mtazamo wa maendeleo zaidi na ishara Singida itapata
mabadiliko makubwa ya kiuchumi.
Amesema kilimo cha
umwagiliaji kina tija zaidi kuliko kutegemea mvua pekee ambapo Singida
inajipanga kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula nchini huku ikiwa na lengo la
kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya makao makuu ya nchi ambayo maeneo
mengi yatakuwa na shughuli za kiofisi zaidi.
Dkt Nchimbi
amesisitiza Mkoa wa Singida hauna njaa, sio masikini na wala sio kame na
wananchi wa singida wamejipanga kutumia fursa zozote zinazojitokeza kwa ajili
la kukuza uchumi.
Aidha amewataka
wananchi wa Singida kufanya kazi kwa bidii ili kujiongezea kipato na kuwa
washiriki wakubwa katika kuelekea uchumi wa kati na wa viwanda.
0 comments:
Post a Comment