Na Mwandishi wetu kutoka Zanzibar.
Mh Hamad Yussuf Masauni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Mh Nassoro Jazira Muwakilishi wa Jimbo la Kiwajuni pamoja na madiwani wao jana walikuwa na ugeni wa madaktar bingwa wa maradhi mbali mbali mbali.
Wataalamu hao walikuwa kituo cha afya cha Rahaleo kwa ajili ya kupima kuchunguza na kutibu bure maradhi mbali mbali kwa wananchi wa Jimbo la Kikwajuni na Majimbo jirani waliojitokeza.
Madaktari hao ni wataalamu wa Maradhi ya Mifupa Kifua Kikuu Presha Mgongo Tezi dume Shinikizo la damu.
*Program hiyo ni muendelezo wa utekelezaji ila ya CCM na ahadi za viongozi hao wa Jimbo la Kikwajuni walizoweka wakati wa kamapeni*
Jimbo la Kikwajuni kwa upande wa afya pia limeazisha mfuko wa bima ya afya bure kwa wazee na tayari zaidi ya wazee 2034 wameshapatia vitambulisho na wanapata matibabu bure.
Wakati zoezi hilo la upimaji wa afya likiendelea viongozi wa Jimbo hilo walipata fursa ya kusema machache.
Tunawapongeza wananchi wa kikwajuni kwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao MH MASAUNI
Tunachokifanya Leo ni muendelezo wa ahadi zetu na kuitekeleza ilani ya ccm ya 2015 _2020 MH MASAUNI
Tumekubaliana na MH MASAUNI na kwa kushirikiana na mfuko wa barabara kuitia lami njia inayoingilia katika kituo cha afya rahaleo ili wananchi wasipate tabu ya njia wakati wa kuja kituoni MH JAZIRA
Uwepo wa madaktari hawa mabingwa kutoka Tanzania bara na India ni matunda ya muungano wetu na mashirikiano mazuri na mataifa mengine MH MASAUNI
Umoja na mshikamano wa wananchi wa kikwajuni na mashirikiano wanayotupa sisi viongozi wao ndio yanayopelekea kuitekeleza kirahisi ilani ya uchaguzi ya ccm pamoja na ahadi tulizozitowa kipindi cha uchaguzi MH MASAUNI
Leo katika upimaji wa afya kwa wananchi wa jimbo la kikwajuni wamepata fursa ya kupima na kutibiwa bure.
MH MASAUNI.
Tunawapongeza viongozi wezetu Madiwani wa wadi zote mbili kwa kuhamasisha vizuri wananchi wakaweza kujitokeza kwa wingi Pia tunawashukuru kwa kuwa karibu na sisi kwa kila jambao la ushauri na utekelezaji na ndio maana leo tupo sote kwa shuhuli hii.
MH MASAUNI.
0 comments:
Post a Comment