Na Mwandishi wetu kutoka Zanzibar
Mh Salum Ussi Pondeza (AMJADI) leo amekutana na zaidi ya watoto yatima mia tano na watoto wenye mahitaji maalum wanaoishi ndani ya Jimbo lake LA Chumbuni.
Taasisi ya PONDEZA Foundation kila mwaka imekuwa ikifanya jambo hili ifika sikukuu ya mosi Mfunguo tatu na hufanya hivyo kwa lengo la kuwafariji watoto yatima ili wajuwe binaadamu site sawa na waweze kuondokana na mawazo ya kuwa wapweke.
Watoto hawa wapo chini ya kituo cha PONDEZA foundation kwa uangalizi maalum na Mara baada ya kutimiza miaka 18 huwaruhusu wakaaze maisha ya kujitegemea hiyo ni baada ya kuwa kushawapa mbinu za kupambana na maisha na mafunzo mbali mbali ya stadi za maisha alisema MH Amjadi.
Katika hafla hiyo watoto hao waliongoza na wazazi wao na wananchi wa Jimbo la Chumbuni pamoja na viongozi mbali mbali wa Chama na Serekali walialikwa.
Pamoja na Mkono wa IDDI kwa watoto pia kulisomwa dua ya kuwarehemu waliotangulia kuwaombea dua wagonjwa na kuiombe dua nchi Mwenyezi Mungu ailinde na ibaki kuwa na amani na utulivu.
0 comments:
Post a Comment