
Mkuu
wa wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo, akitembelea banda la VETA katika
maonesho ya Kilimo 2017 yanayoendelea mkoani Lindi katika viwanja vya
Ngongo ambapo alipongeza VETA kwa kuweka fursa nyingi za mafunzo ya
ujuzi kwa makundi mbalimbali ya wananchi. Aliahidi kushirikiana na VETA
ilikuwa wezesha wananchi wilaya ni kwake kunufaika pia na fursa
mbalimbali za mafunzo ya ufundi stadi.

Wanafunzi
wa shule ya sekondari Medi ya mkoani Mtwara wakipata maelekezo juu ya
aina ya mafunzo yanayotolewa katika vyuo vya ufundi Stadi walipotembelea
banda la VETA katika Maonyesho ya kilimo ya Nanenane yanayofanyika
kitaifa katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Mwalimu
wa Elektroniki wa Veta Kipawa, Aneth Mganga akiwapa maelezo wananchi
waliotembelea banda la VETA Pikipiki inayoendeshwa ni lazima dereva awe
amevaa kofiangumu.

Wananchi wakipata maelezo ya jiko la mafuta ya taa ambalo limebuniwa kwa kutotumia mafuta mengi na halina moshi.

Baadhi
ya wananchi waliofika kutembelea banda la VETA ili kuweza kupata
taarifa mbalimbali kuhusianana VETA pamoja na kuaangalia teknolojia
mbalimbali.
Katika kukabiliana na
changamoto za madhara ya ajali za pikipiki yanayosababishwa na madereva
kutovaa kofiangumu (helmet), Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
(VETA) imebuni teknolojia ya kukabiliana na hilo.
Mwalimu wa fani
ya elektroniki kutoka VETA Kipawa, AnethMganga, amebuni mfumo wa
kielektroniki unaozuia pikipiki kuwa kampaka dereva awe amevaa
kofiangumu (helmet).
Akizungumza na katika viwanja vya maonesho ya
Nanenane Ngongo, mkoani Lindi, mwalimu Aneth amesema mfumo huo ukianza
kutumika na madereva wa pikipiki utapunguza madhara endapo kunatokea
ajali kwa kuwa bila ya kuvaa kofiangumu pikipiki haiwaki na hata ukiwa
katika mwendo ikitokea ukavua kofiangumu pikipiki itazimika.
Aidha,
katika usalama barabarani inasaidia kuzuia wizi wa pikipiki kwani mwizi
hatoweza kuiwasha bila kofiangumu ambayo imeunganishwa kieletroniki.
Aneth
amesema anaendelea kufanya utafiti nakuboresha zaidi ubunifu huo,
lakini ameomba serikali na wadau mbalimbali kuunga mkono ili uweze
kuenea, kukubalikana kutumika na waendesha pikipiki katika maeneo
mbalimbali nchini.
0 comments:
Post a Comment