Rais
wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amesema ikiwa atashindwa kwa haki, Uchaguzi
Mkuu wa tarehe nane mwezi Agosti, atakubali matokeo na kukabidhi
madaraka kwa amani.
Rais
Kenyatta ametoa hakikisho hilo wakati akijibu maswali mbalimbali
kupitia runinga na kumtaka mpinzani wake Raila Odinga, naye kuwa tayari
kufanya hivyo ikiwa atashindwa katika Uchaguzi huo.
Kenyatta amesisitiza kwamba, yeye ni mtu anayeheshimu uamuzi wa wananchi, na kuwaomba wapinzani wake nao wafanye hivyo.
Aidha,
amesema serikali yake imelenga Uchaguzi huo uwe wa amani ndiyo maana
maafisa wa usalama wamejihami na wako tayari kukabiliana na wale
watakaotaka kuzua fujo.
Naye
Bw. Odinga, anayepeperusha bendera ya muungano wa upinzani NASA,
amekuwa akisema kuwa atakubali matokeo hayo ikiwa Uchaguzi huo utakuwa
huru na haki.
Hata
hivyo, hivi karibuni ametoa madai mazito kuwa Rais Kenyatta anatumia
jeshi kumsaidia kuiba kura, madai ambayo serikali imekanusha.
0 comments:
Post a Comment