Rais
John Magufuli amewaahidi wakaazi wa mkoa wa Tanga kuwa serikali yake
itapanua bandari ya Tanga na kuhakikishia ina uwezo wa kufikiwa na meli
kubwa zitakazokuwa zikisafirisha mafuta yatayovunwa kupitia bomba
linalotarajiwa kujengwa kutoka Hoima nchini Uganda hadi jijini humo.
Akiuhutubia
umati wa wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa mradi huo
uliofanyika eneo la Chongoleani akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda,
Yoweri Museveni, Rais Magufuli alisema kuwa amesikia kilio cha wananchi
wa Tanga kupitia kwa Mkuu wa Mkoa huo na kwamba atalifanyia kazi kwa
vitendo.
“Haiwezekani
tukawa na mahali ambapo meli kubwa-kubwa zinakuja kwa ajili ya kuchukua
mafuta ghafi halafu kina cha maji kiwe kidogo. Kwahiyo, tutapanua pia
bandari ya Tanga ili tuwe na bandari tatu kubwa,” amesema Rais Magufuli.
“Kama
tunavyopanua bandari ya Mtwara, kama tunavyopanua bandari ya Dar es
Salaam na bandari ya Tanga tutaipanua ili kina chake kiongezeke; ili
wananchi wa Tanga waweze kufanya biashara,” aliongeza.
Katika
hatua nyingine, Rais Magufuli pia aliahidi ujenzi wa barabara mpya
itakayounganisha jiji la Tanga na Bagamoyo ambayo itaratibiwa na jumuiya
ya Afrika Mashariki.
Rais
Magufuli na Rais Museveni wanazindua ujenzi wa bomba la mafuta ghafi
kutoka Ohima nchini Uganda hadi mkoa wa Tanga, ujenzi unataorajiwa
kuchukua takribani miaka mitatu
0 comments:
Post a Comment