Shirika
moja la kutetea wanyama nchini Kenya limesema bei ya Punda imepanda
maradufu nchini humo kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya nyama ya
mnyama huyo nchini China taifa ambalo hununua kwa wingi bidhaa ya mnyama
huyo.
Kwa
mujibu wa shirika hilo, sababu ya bei ya Punda kupanda kwa karibu 200%
ni kutokana na ongezeka la biashara ya bidhaa za mnyama huyo huko Uchina
ambako nyama ya punda ni kitoweo kilicho na walaji wengi.
Mataifa
kadhaa ya Afrika yamepiga marufuku uuzaji wa nyama na bidhaa nyinginezo
za punda, nchini China kwa sababu mnyama huyo ambae hutumiwa zaidi kwa
ajili ya kusaidia kubeba mizigo mashambani, sasa idadi yao inapungua kwa
kasi mno.
Baadhi
ya Mataifa ya Afrika yaliyopiga marufuku uchinjaji na uuzaji wa nyama
ya Punda ni pamoja na Uganda, Tanzania, Botswana, Niger, Burkina Faso,
Mali, na Senegal.
0 comments:
Post a Comment