Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam Paul Makonda akitazama mambo ya kupitishia maji ikiwa ni pia
sehemu ya miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo
wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Paul Makonda akipewa maelezo mafupi juu ya muundo mzma mzima wa miundo
mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa
maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Paul Makonda akitazama miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika
kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa
jiji la Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Paul Makonda akishiriki kuchimba mtaro wa kupitisha bomba la maji
ikiwa ni sehemu ya miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake
kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la
Dar.
……………………………………………………………………
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul
Makonda leo amefanya ziara ya ukaguzi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji
ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa Maji ya
kutosha kwa Wakazi wa Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo Makonda
ametembelea Ujenzi wa Vituo vya Usambazaji wa Maji, Visima pamoja na
maeneo yatakayojengwa mifumo ya kisasa ya kusafirisha na kutibu Maji
taka.
Makonda amesema lengo
la Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli ni kumtua Mama Ndoo
kichwani na kuhakikisha huduma ya Maji inawafikia Wananchi wote.
Amesema kukamilika
kwa miradi ya Ujenzi wa Vituo Vinne vikubwa vya usambazaji wa Maji
vinavyojengwa maeneo ya Changanyikeni, Makongo, Wazo na Bunju*vitasaidia
kuzalisha Maji ya kutosha na kutatua kero kwa Wananchi.
Katika ziara hiyo pia Makonda
ametembelea Visima 10 ambavyo aliahidi kwenye Ziara ya Dar Mpya ambavyo
Ujenzi wake umekamilika vikiwa na uwezo wa kuzalisha Lita 16,000 kwa
kila kisima ambavyo vitahudumia wakazi wa Wilaya ya Ubungo.
Aidha Makonda ametembelea eneo la Jangwani ambapo kutajengwa
Mfumo wa Maji taka utakaogharimu kiasi cha Bilion 200 na eneo la
Kilongawima Mbezi Beach kunakojengwa mfumo wa Maji taka utakaogharimu
kiasi cha Bilion 135 chini ya ufadhili wa Bank ya Dunia na Serikali ya
Japan.
Hata hivyo amesema
bado Serikali inaendelea kufanya jitiada za kuhakikisha Wakazi wa Wilaya
ya Kigamboni na Temeke wanapata maji ya kutosha kupitia miradi
mbalimbali inayoendelea.
Amewataka Wananchi
ambao bado hawajaunganishwa na huduma ya Maji kufika Ofisi za DAWASCO
ili waunganishiwe Maji bila malipo ambapo baada ya hapo watawekewa
utaratibu wa malipo.
0 comments:
Post a Comment