METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, August 10, 2017

NBS YATANGAZA HALI YA MFUMUKO WA BEI KWA TAIFA ULIVYO SASA


Ephraim Kwesigabo Mkrugenzi wa sensa na takwimu za jamii.

Mfumuko wa bei wa bei wa taifa kwa mwezi Julai,2017 umepungua  hadi kufikia asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 5.4 iliyokuwa mwezi juni mwaka huu.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioulioishia mwezi julai 2017 imepungua ikilinganishwa na mwezi juni mwaka 2017.

Taarifa hiyo imetoewa na  Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa ,wa ofisi ya Takwimu , Dar es salaam ambapo ameeleza  kupunguwa kwa mfumuko wa bei wa mwezi julai 2017 kumechangiwa hasa na kupunguwa kwa bei za bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi julai,2017 zikilinganishwa na bei za mwezi julai,2016.

Hata hivyo imeelezwa kuwa baadh ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na Nyama kwa asilimia 3.8, samaki wabichi asilimia 14.1, dagaa kwa asilimia 8.4,kabichi kwa asilimia 16.6,biringanya kwa asilimia 10.6, vitunguu kwa asilimia 13.2, karoti kwa asilimia 16.9,njegere kwa asilimia 15.7 na viazi mviringo kwa asilimia  13.5.
 
Aidha thamani ya shilingi ya Tanzania imezidi kuimarika ambapo uwezo wa shilingi 100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 91 na senti 87 mwezi julai,2017 ikilinganishwa na shilingi 91 na 66 iliyokuwa mwezi juni.

Mfumuko wa bei nchini Tanzania unamwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za afrika afrika mashariki ambapo nchini Kenya mfumuko wa bei wa mwezi julai,2017 umepungua hadi asiliia 7.47 kutoka asilimia 9.21 mwezi juni,2017 na nchini kenya uganda umepungua hadi asilimia 5.70, mwezi julai 2017 kutoka  asilimia 6.4 mwezi julai juni,2017.

Mfumuko huo wa bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa za huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com