Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Hussein Ruhava
WANAFUNZI wa shule za msingi na sekondari mkoani Kigoma, wametakiwa kutumia maktaba kusoma vitabu na machapisho mbalimbali kwenye maktaba hizo, kuongeza ufahamu na uelewa wa mambo mbalimbali yanayohusiana na masomo yao.
Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Hussein Ruhava ametoa kauli hiyo katika kongamano la kushindanisha wanafunzi kusoma, lililoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Kigoma Women Development Group (KIWODE).
Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Diwani wa Kata ya Kasingirima, Nassoro Hamduni alisema kwa wanafunzi kutumia muda wao wa ziada kusoma vitabu na machapisho mbalimbali yanayohusu masomo yao baada ya muda wa mafunzo darasani, kuna nafasi kubwa ya kuwawezesha wanafunzi kufanya vizuri kwenye masomo yao.
Akisoma risala ya kongamano hilo, Mwenyekiti wa Kiwode, Sophia Patrick alisema pamoja na kuongeza ari ya wanafunzi kupenda na kuongeza uwezo wao wa kusoma, pia kongamano hilo linatumika kuwaweka pamoja wadau wa elimu kujadili changamoto zinazowakabili na hatua za kuchukua kulingana na nafasi zao na rasilimali zinazowazunguka.
0 comments:
Post a Comment