Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Elimu Solutions, Neithan Swed akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.
Anthony Mtaka tuzo ya elimu iliyotolewa na Taasisi hiyo kwake ikiwa ni
kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango
mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu,
Komredi Enock Yakobo akionesha tuzo ya elimu iliyotolewa na Taasisi ya
Elimu Solutions kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ikiwa ni
kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango
mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu.
******************
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa Mkoa wa Simiu, Mhe.
Anthony Mtaka amepewa tuzo ya elimu ya Tanzania Elimu Awards na Taasisi
ya Elimu Solutions, ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi
aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu
Mkoani Simiyu.
Tuzo hiyo imekabidhiwa na
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Solutions, Neithan Swed, Mjini
Bariadi wakati wa uzinduzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato
cha nne waliopata ufaulu hafifu(daraja sifuri) katika mtihani wa Mock
kwa lengo la kuwasaidia kuongeza ufaulu wao katika Mtihani wa Taifa
utakaofanyika mwezi Novemba 2019.
Swed amesema Taasisi hiyo
imefuatilia na kuona juhudi zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
katika mapinduzi ya elimu ikiwemo ubunifu wa kuanzisha kambi za
kitaaluma ambazo zimeonekana kuwa na mchango mkubwa katika kuongeza
ufaulu wa mkoa wa Simiyu kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kutoka
mwaka 2016 hadi mwaka 2018.
“Anayoyafanya Mhe. Mtaka
hayaishii Simiyu peke yake Tanzania inayaona, tulifuatilia habari za
kambi za kitaaluma na tukaangalia nafasi ya mkoa katika matokeo na namna
mlivyofanya vizuri, mmeweka alama kwenye Taifa na tunatamani Mhe. Mtaka
aziendeleze juhudi hizi zaidi ili mtoke kwenye kumi bora mwende tatu
bora na mwakani tupate mwanafunzi bora kutoka Simiyu atakayepata tuzo
hii” alisema Neithan Swed.
Katika hatua nyingine Swed
amesema Taasisi ya Elimu Solutions itatoa ufadhili kwa mwanafunzi wa
kidato cha nne mwaka 2019 atakayefanya vizuri katika mtihani wa Taifa na
kumpeleka nchini China kuendelea na masomo.
Akipokea tuzo hiyo Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Taasisi ya Elimu
Solutions kwa kutambua juhudi zinazofanywa na mkoa wa Simiyu na kutoa
tuzo huku akibainisha kuwa mkoa wa Simiyu unaithamini sana tuzo hiyo.
Aidha, Mtaka ameipongeza
Taasisi ya Elimu Solutions namna wanavyohamasisha maendeleo ya Elimu ya
Watanzania ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili kwa wanafunzi wanaofanya
vizuri kwenda kusoma nje ya nchi.
Tuzo za Elimu Tanzania Elimu
Awards zimetolewa na Taasisi ya Elimu Solutions kwa wadau mbalimbali wa
elimu waliochangia na kusaidia kuleta mabadiliko kwa ubunifu na juhudi
zao binafsi, taasisi zinazoihudumia sekta ya elimu; pia hutolewa kwa
viongozi, walimu, wanafunzi waliofanya vizuri kwenye elimu
0 comments:
Post a Comment