Na Mathias Canal, Dar es salaam
Halmashauri ya Manispaa ya ya Ubungo Jijini Dar es salaam imezipiku Manispaa zote za Jiji la Dar es salaam zikiwemo Kinondoni, Ilala, Temeke na Kigamboni kwa kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya Afya na usafi wa Mazingira kwa mwaka 2017.
Kwa mujibu wa wa Taarifa iliyotolewa leo Agosti 11, 2017 na Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, jinisia, wazee na watoto imebainisha kuwa Manispaa ya mpya ya Ubungo kuwa bingwa katika mchuano huo pamoja na kuanza kwake hivi karibuni.
Katika taarifa hiyo iliyoifikia www.wazo-huru.blogspot.com imebainisha kuwa pamoja na Manispaa ya Ubungo kushika nafasi ya kwanza Kimkoa lakini pia imekuwa Manispaa bora zaidi katika maswala ya Afya, na Usafi wa mazingira kwa kuzipiku Halmashauri zote zilizopo katika Mkoa wa Pwani na Dar es salaam.
Akizungumzia ushindi huo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ameeleza kuwa ushirikiano mkubwa kati yake na watumishi wote katika Manispaa ndio njia pekee ya mafanikio iliyopelekea mafanikio hayo makubwa.
Alisema Halmashauri ya Manispaa hiyo inajipanga zaidi kimkakati ili kuongeza ufanisi wa utendaji jambo ambalo litapelekea Manispaa hiyo kushika nafasi ya kwanza katika kipindi cha hivi karibuni.
Kayombo alisema kuwa Mtazamo wa Halmashauri ni kuwa na jamii ambayo
imewezeshwa kuendana na maendeleo ya kijamii, kiuchumi na Miundo mbinu hivyo mafanikio ya kila hatua ni nidhamu bora katika utendaji kwa watumishi wote.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment