Msanii Agnes Gerald maarufu Masogange, anayetuhumiwa kutumia dawa za kulevya amekutwa na kesi ya kujibu.
Uamuzi
huo umetolewa leo Agosti 31, na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele
ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, baada ya upande wa Jamhuri
ukiongozwa na Wakili wa Serikali Constatine Kakula, kufunga ushahidi wao
kwa mashahidi watatu.
Mashahidi
wa upande wa Jamhuri waliotoa ushahidi kwenye kesi hiyo ni Mkemia Elias
Mulima kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye alipima sampuli
ya mkojo na maofisa wawili wa polisi ambao walimpeleka Masogange kwa
mkemia.
Baada
ya kutolewa kwa uamuzi huo, Masogange ambaye anatetewa na Wakili Reuben
Simwanza, alidai atajitetea kwa njia ya kiapo na atakuwa na mashahidi
watatu.
Hakimu
Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 12, mwaka huu, kwa ajili ya
utetezi na kusema dhamana ya mshitakiwa inaendelea.
Masogange
anadaiwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, maeneo yasiyofahamika Dar
es Salaam, alitumia dawa aina ya heroin na Oxazepam.
0 comments:
Post a Comment