MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi ya
wabunge wanane wa Chama cha Wananchi (CUF) waliovuliwa wadhifa huo
walioomba mahakama itoe zuio kwa Bunge kuwaapisha wabunge wapya hadi
kesi ya msingi itakaposikilizwa, kwa kuwa walitumia kifungu cha sheria
kisicho sahihi.
Kutokana na uamuzi huo, muda wowote Bunge litakapowahitaji wabunge
hao wateule wa viti maalumu walioteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) kuapishwa, linaweza kufanya hivyo.
Akisoma uamuzi huo jana, Jaji
Lugano Mwandambo alisema upande wa Serikali uliwasilisha pingamizi tatu
dhidi ya maombi hayo ikiwemo la upungufu wa kisheria ambayo
yaliwasilishwa na waombaji.
Alisema waombaji walitumia sheria ya Uingereza bila kuambatanisha
kifungu cha sheria za hapa nchini ambacho kinaruhusu maombi hayo
kusikilizwa mahakamani hapo. Alisema wanakubaliana na pingamizi
zilizotolewa na upande wa Serikali hususani lililoonesha kwamba waombaji
wametumia kifungu kisicho sahihi, hivyo wanatupilia mbali maombi hayo.
Wakili wa Bodi ya Wadhamini wa CUF, Mashaka Ngole alidai kuwa kesi ya
msingi itasikilizwa Septemba 30 mwaka huu na kwamba bado hawajapeleka
utetezi wao, pia wataangalia ni gharama gani walizotumia kwa ajili ya
kesi hiyo ili waweze kulipwa kwa usumbufu waliopatiwa. Kabla ya kesi
hiyo kutolewa uamuzi, saa 4 asubuhi wanaodaiwa kuwa wanachama wa CUF
upande wa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na wale
wanaomuunga mkono Katibu Mkuu, Maalim Seif Shariff Hamad walianza
kurushiana makonde mahakamani hapo huku sababu za kupigana kwao
hazikufahamika.
Kutokana na hali hiyo, askari polisi zaidi ya sita waliokuwa
mahakamani hapo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi walifika katika ukumbi wa
mahakama hiyo na kuanza kuzungumza na wanachama hao kwa lengo la
kupunguza ghasia na baadaye hali ilirudi kuwa shwari. Awali, wakati wa
kusikilizwa maombi hayo, miongoni mwa pingamizi zilizowasilishwa na
Malata ni kuwa kuwa maombi hayo hayatekelezeki kwa kuwa yanalenga kuzuia
majukumu ya Bunge ambayo yameainishwa kwa mujibu wa Ibara ya 68 ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Malata ambaye alikuwa akiongoza jopo la mawakili wa serikali, alidai
waombaji hao wanatumia mamlaka za aina mbili kupata haki zao mojawapo ni
kupitia utaratibu wa kichama ambapo walikata rufaa ndani ya Mkutano
Mkuu kupinga maamuzi ya baraza na pia wanatumia mahakama kutafuta haki
hizo hizo ambazo wangeweza kuzipata kupitia chama chao.
Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alipinga hoja
zilizotolewa na upande wa Serikali akidai kuwa hazina msingi kwa kuwa
kifungu cha sheria ambacho wateja wao waliegemea kuleta maombi hayo,
kinaipa mamlaka mahakama kutoa maamuzi. Waombaji katika kesi hiyo ambao
walikuwa wabunge kabla ya kuvuliwa uanachama na kupoteza nafasi hizo ni
Miza Bakari, Savelina Mwijage, Salma Mohammed, Raisa Abdallah na Riziki
Mngwali, Hadija Salum Al- Qassmay, Halima Ali Mohamed na Saumu Heri
Sakala wakati madiwani ni Elizabeth Magwaja na Layla Hussein.
Katika maombi hayo wadaiwa ni Bodi ya Wadhamini wa CUF, Tume ya
Uchaguzi (NEC), katibu wa Bunge na wabunge wapya walioteuliwa na NEC.
Julai 27 mwaka huu, NEC kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na
kifungu cha 86(8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343,
iliwateua Rukia Kassim, Shamsia Mtamba, Kiza Mayeye, Zainab Mndolwa,
Hindu Mwenda, Sonia Magogo, Alfredina Kahigi na Nuru Bafadhili kuwa
wabunge wa Viti Maalumu katika Bunge la Muungano, wakichukua nafasi ya
waliofukuzwa na chama chao.
Jana jioni, saa chache baada ya uamuzi wa Mahakama, upande wa wabunge
waliotimuliwa CUF na kuvuliwa ubunge, kupitia Wakili Kibatala
waliwasilisha maombi mapya Mahakama Kuu kulizuia Bunge lisiwaapishe
wabunge wapya. Katika maombi hayo, wameongezwa walalamikiwa ambao ni
Wakurugenzi wa Manispaa za Temeke na Ubungo, kutokana na madiwani wawili
waliokuwa miongoni mwao kutimuliwa.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad
amekwama kutimiza azma ya kuwaondoa bungeni wabunge wawili wa chama
hicho, Magdalena Sakaya wa Kaliua na Maftaha Nachuma wa Mtwara Mjini,
baada ya taarifa ya Spika jana kueleza kuwa, anasita kuifanyia kazi
barua ya Maalim Seif ya kuwatimua wabunge hao kutokana na taarifa za
awali alizopokea kuonesha kuwa, kuna mabadiliko ndani ya uongozi wa
chama hicho yanayomtambua Sakaya kuwa ndiye anayetekeleza majukumu ya
Katibu Mkuu wa chama hicho kwa sasa, badala ya Maalim Seif.
“Ofisi ya Spika inayo barua ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha CUF,
Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba yenye Kumbukumbu Namba CUF/AK/DSM/
MKT/05/2017 ya Machi 22, 2017 ikiliarifu Bunge kuwa Maalimu Seif Shariff
Hamad ameshindwa kutekeleza majukumu yake kama Katibu Mkluu, hivyo kwa
mujibu wa Katiba ya CUF, majukumu ya Katibu Mkuu yanatekeleza kuanzia
tarehe hiyo na Magdalena Sakaya,” imesema sehemu ya barua hiyo.
Aidha,
imesema barua hiyo ilikuwa na kiambatanisho cha ridhaa ya mabadiliko
hayo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na kwamba Ofisi ya Spika haijawahi
kupokea barua yoyote ikieleza vinginevyo.
Saturday, August 5, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. William Sam...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya kilim...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki zoezi la upandaji wa mbegu za pamba kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya mji wa Geita. Mkuu wa Mkoa wa Geita,akiwasili kwenye eneo la shamba na kusalimiana na viongozi wa halmashauri hiyo akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi.
Afisa Kilimo wa halmashauri ya mji,Bw Samwel Ng'wandu akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga.
Baadhi ya watumishi na Jeshi la akiba (MGAMBO)wakishiriki shughuli za kupanda mbegu kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya mji.
Wataalamu wa kilimo mkoani Geita wametakiwa kuwafuatilia kwa karibu wakulima wa pamba na kuwaelekeza kulima kwa tija ili kuzalisha zaidi tofauti na miaka ya nyuma.
Akizindua msimu wa kilimo cha pamba kwenye mashamba ya watumishi wa Halmashauri ya mji wa Geita yaliyoko kata ya Buhalahala ,Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema ni vema wataalam hao wakafika kwenye maeneo ya kilimo na kuwaelekeza wakulima kanuni zitakazowasaidia kuvuna pamba nyingi.
“Wito wangu kwa wakulima wote pamoja na wataalam wetu wa kilimo baada ya uzinduzi huu mkubwa kabisa wa kilimo cha pamba Mkoani kwetu,wataalam ni vyema wakawasaidia wakulima kufuata zile kanuni kumi bora za kilimo ambacho kitaweza kuwa saidia wakulima lakini nataka twende kisayansi zaidi”Alisema Luhumbi.
Mhandisi Luhumbi Aliongezea Kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kumsaidia mkulima na kuwataka wakulima kuchangamkia fursa hiyo na kuwekeza katika sekta ya kilimo cha pamba kwa kuwa hali ya hewa ya mwaka huu ni nzuri.
Mshahuri wa kilimo cha Mkataba Mkoani Geita Bw Joshua Mirumbe alisema lengo ni kuhakikisha wanaongeza tija ya uzalishaji kutoka wastani wa kilo 250 hadi 300 na kwenda kwa wastani wa kilo 800.
Katika msimu wa mwaka 2016/2017 mkoa wa Geita ulilenga kulima hekta 67002 zilizotarajiwa kuzalisha tani ,93437 za pamba lakini utekelezaji ulikuwa hekta 24 791 zilizozalisha tani 13 267.8 zenye thamani ya Sh Bilioni 15.Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki zoezi la upandaji wa mbegu za pamba kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya ...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment