Ikiwa
ni siku chache kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini Kenya, Muungano
wa Upinzani (NASA) umeishutumu serikali kuwa imevamia moja ya vituo
vyake vya kuhesabia kura kilichopo eneo la Westlands jijini Nairobi.
Msemaji
wa NASA ameeleza kuwa wanaume waliokuwa wamefunika nyuso zao walivamia
ofisi hiyo wakafanya uharibifu na kubeba kompyuta, simu za mkononi na
vitabu.
Kwa
upande wake, serikali ya nchi hiyo imesisitiza kuwa hakuna uvamizi
uliofanyika, . Mgombea wa upinzani Raila Odinga amesema kuwa atakubali
tu kushindwa ikiwa uchaguzi utakuwa wa haki.
Hivi
karibuni, Rais wa Uhuru Kenyatta alikaririwa akisema ataheshimu matokeo
ya uchaguzi huo wa siku ya Jumanne licha ya kila mmoja kusisitiza kuwa
ataibuka mshindi.
Uchaguzi
wa Kenya mara nyingi umekua ukikumbwa na ghasia. Zaidi ya watu 1000
waliuawa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
0 comments:
Post a Comment